Kigawe
Mandhari
Kigawe (ing. multiple) ni namba kubwa inayoweza kugawanywa kwa namba ndogo.
Mfano: 30 ni kigawe cha 10.
Kigawe kidogo cha shirika cha namba m na n ni nambakamili ndogo ambayo ni nambachanya na kigawe cha m , pia kigawe cha n.
Mfano wa 12 na 18:
- Vigawe vya 12 ni 12, 24, 36, 48, 60, 72, 84, 96, 108, …
- Vigawe vya 18 ni 18, 36, 54, 72, 90, 108, …
- Vigawe vidogo vya shirika vya 12 na 18 hivi ni 36, 72, 108, …
- Kigawe kidogo cha shirika ni 36.