Penalti
Penati , pia penalti (ing. penalty) ni istilahi ya lugha ya michezo, hasa mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa pete n.k. .
Penati ni nafasi ya mchezaji mmoja kupiga mpira kwa goli ya wapinzani kutoka nukta iliyopo mita 11 mbele ya goli. Hapa hawezi kushambuliwa au kuzuiliwa na mchezaji mwingine.
Nafasi hii inatolewa kama mchezaji wa timu inayotetea goli yake anafanya kosa katika eneo la penalti ambalo ni eneo karibu na goli (kwa mpira wa mguu umbali wa mita 16.5). Penalti mara nyingi inaleta goli kwa hiyo inaweza kuamulia matokeo ya mchezo. Hapo kupata penalti ni kama adhabu kwa timu iliyotetea goli yake kwa kukosea kanuni za michezo.
Kusudi lake ni kuzuia matumizi ya mbinu zisizo halali katika eneo muhimu karibu na goli.
Kwenye mashindano makubwa ya soka penati inatumiwa pia kama njia ya kumpata mshindi kama mchezo unaishia kwa sare (droo). Hapa kila timu inapewa nafasi 5 kupiga mpira kutoka nukta ya penati yaani kwa umbali wa mita 11. Kama tokeo ni sare tena yote hurudiwa hadi timu moja iko mbele na hivyo kuwa mshindi.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |