Emau
Emau ni mji uliotajwa katika Injili ya Luka katika Agano Jipya. Mwinjili Luka anaandika kua Yesu alionekana huko baada ya Mauti na Ufufuko wake mbele ya Mitume walipokua wakitembea katika njia iliyoelekea Emau.
Utambulisho wake wa kijiografia sio wazi, maeneo kadhaa yamependekezwa katika historia. Inajulikana tu kwamba ilikuwa imeunganishwa na barabara ya kwenda Yerusalemu ; umbali uliotolewa na Mwinjili Luka unatofautiana katika hati tofauti na takwimu iliyotolewa imefanywa konekana ngumu zaidi na watafsiri.
Jina
Jina la mahali Emau ni la kawaida katika vyanzo vya zamani juu ya Levant na kawaida hutoholewa kutoka lugha ya Kigiriki na Kilatini kutoka kwa neno la Kisemiti la "chemchemi ya joto", kwa Kiebrania ni hamma au hammat (חמת). Katika Mashariki ya Kati ya zamani na ya leo, tovuti nyingi zinaitwa Hama Hamath na tofauti zake. [1]
Kwa sasa inadhaniwa kujulikana kama ni Motza.
Emau katika Agano Jipya
Luka 24: 13-35 inahubiri kwamba Yesu anaonekana baada ya kufufuka kwake kwa wanafunzi wawili ambao wanatembea kutoka Yerusalemu kwenda Emau, ambayo inaelezewa kuwa ni stadiia 60 (10.4 hadi 12 km kulingana na ufafanuzi gani wa stadion unatumika) kutoka Yerusalemu. Mmoja wa wanafunzi anaitwa Kleopa (aya ya 18), wakati mwenzake hajatajwa jina.