Nenda kwa yaliyomo

Bhutan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
'འབྲུག་ཡུལ
Druk Gyal-khab
Brug Rgyal-khab

Dru Gäkhap

Ufalme wa Bhutan
Bendera ya Bhutan Nembo ya Bhutan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Nchi moja, taifa moja"
Wimbo wa taifa: Druk tsendhen
Lokeshen ya Bhutan
Mji mkuu Thimphu
27°28′ N 89°38′ E
Mji mkubwa nchini Thimphu
Lugha rasmi Dzongkha
Serikali Ufalme
Jigme Khesar Namgyal Wangchuck
Lotay Tshering
Formation
Wangchuk Dynasty
17 Desemba 1907
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
38,394 km² (ya 136)
1.1
Idadi ya watu
 - 2012 kadirio
 - 2006 sensa
 - Msongamano wa watu
 
742,737 (ya 165)
672,425
18/km² (ya 196)
Fedha Ngultrum (BTN)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
BTT (UTC+6:00)
(haitumiki) (UTC+6:00)
Intaneti TLD .bt
Kodi ya simu +975

-


Ramani ya Bhutan

Bhutan ni nchi ndogo ya Bara Hindi katika milima ya Himalaya.

Nchi imepakana na Uhindi na jimbo la Tibet la China.

Imetawaliwa na mfalme Jigme Singye Wanchuck tangu 1972.

Kuna wakazi takriban lakhi saba unusu.

Mji mkuu unaitwa Thimphu.

Jiografia

Bhutan ni nchi ya milima, na zaidi ya 80% za eneo la Bhutan ziko juu ya kimo cha mita 2,000. Kusini tu kuna kanda nyembamba ya tambarare ya Duar.

Watu walio wengi hukalia eneo la milimani kati ya mita 2,000 hadi 3,000 juu ya UB.

Mpakani kwa China kuna milima ya juu ya Lunana. Kula Kangri ni mlima mkubwa wenye kimo cha mita 7,553.

Zaidi ya theluthi mbili za nchi zimefunikwa na misitu.

Historia

Bhutan ilianzishwa mwaka 1644 na mmonaki Mbuddha Shabdrung Ngawang Namgyel.

Nchi iliweza kutunza uhuru wake hadi leo, lakini ililazimishwa kukubali maeneo ya kusini yatwaliwe na Waingereza na kuunganishwa na Uhindi wa Kiingereza. Uingereza ilishughulika pia mawasiliano ya nje ya Bhutan.

Uhusiano huu umeendelea na India kulingana na mkataba wa urafiki wa tarehe 8 Agosti 1949.

Tarehe 12 Februari 1971 Bhutan ikapokelewa kama nchi mwanachama wa UM.

Wakazi na Utamaduni

Mbhutan
Ngoma ya kinyago ya Bhutan

Wabhutan walio wengi huishio mlimani wako karibu kiutamaduni na kilugha na watu wa Tibet na Burma. Hao hufuata dini ya Ubuddha (67-75%) ambayo ndiyo dini rasmi. Lugha za jamii hiyo zinazotumika nchini humo ni 23. Mojawapo, Kidzongkha, ndiyo lugha rasmi.

Watu wa kusini wanafanana zaidi na watu wa Nepal na hutumia Kinepali, mojawapo ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Wanafuata dini ya Uhindu (22-33%).

Bhutan inajitahidi kutunza utamaduni wake. Hadi mwaka 1974 watalii hawakuruhusiwa kutembelea nchi. Baadaye imewezekana lakini si rahisi kupata kibali.

Tazama pia

Marejeo

  • Karma Phuntsho (2013). The History of Bhutan. Nodia: Random House India. ISBN 9788184003116.
  • Osmani, Siddiqur R.; Bajracharya, B.B.; Tenzing, S.; Wangyal, T. (2007). Macroeconomics of Poverty Reduction: The Case Study of Bhutan (PDF) (tol. la 2). Colombo: UNDP. uk. 302. ISBN 978-955-1416-00-3. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2011-07-28. Iliwekwa mnamo 2015-10-16.
  • Wangchhuk, Lily (2008). Facts About Bhutan: The Land of the Thunder Dragon. Thimphu: Absolute Bhutan Books. ISBN 99936-760-0-4.
  • Revkin, Andrew C.. "A New Measure of Well-Being From a Happy Little Kingdom", The New York Times, 4 October 2005. Retrieved on 4 October 2005. 
  • "Border tension pushes MEA allocation". The Tribune, Chandigarh. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2005-07-22. Iliwekwa mnamo 8 Septemba 2005. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  • "Bhutan". Bhutan. MSN Encarta. http://encarta.msn.com/encyclopedia_761568123/Bhutan.html. Retrieved 8 September 2005. Archived 28 Oktoba 2009 at the Wayback Machine.
  • "BTI 2008 — Bhutan Country Report". Gütersloh: Bertelsmann Stiftung. 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-24. Iliwekwa mnamo 11 Desemba 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • A.P. Agarwala (2003). Sikkim and Bhutan. Nest and Wings. ISBN 81-7824-008-4.
  • Datta-Ray, Sunanda K. (1984). Smash and Grab: The Annexation of Sikkim. Vikas. ISBN 0-7069-2509-2.
  • Foning, A.R. (1987). Lepcha, My Vanishing Tribe. Sterling Publishers. ISBN 81-207-0685-4.
  • Rose, Leo. The Nepali Ethnic Community in the Northeast of the Subcontinent. University of California, Berkeley.
  • Napoli, Lisa (2011). Radio Shangri-La: What I Learned in Bhutan, the Happiest Kingdom on Earth. Crown. ISBN 0-307-45302-2.
  • Niestroy, Ingeborg; García Schmidt, Armando; Esche, Andreas (2013). "Bhutan: Paradigms Matter", in: Bertelsmann Stiftung (ed.): Winning Strategies for a Sustainable Future. Reinhard Mohn Prize 2013. Verlag Bertelsmann Stiftung, Gütersloh. ku. 55–80. ISBN 978-3-86793-491-6. {{cite book}}: External link in |title= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bhutan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.