Mr Nice
Mandhari
Mr Nice | |
---|---|
Faili:Lucas Mkenda.jpg | |
Taarifa za awali | |
Jina la kuzaliwa | Lucas Mkenda |
Amezaliwa | Moshi, Tanzania |
Kazi yake |
Lucas Mkenda (maarufu kama Mr Nice[1]; Alizaliwa mwaka 1978, Moshi, Tanzania) ni mwimbaji mkongwe wa Tanzania na mmoja wa waimbaji mashuhuri waliotawala muziki wa Afrika Mashariki mwanzoni mwa miaka ya 2000.[2]
Alianza kupata umaarufu mwaka 1999 baada ya kutoa albamu yake ya kwanza, Kidali Po, na kuelekea mwisho wa 2002, alitoa albamu yake ya pili, Rafiki, pia nyimbo zake kama; Kikulacho, Fagilia Wote[3] na Kuku Kapanda Baiskeli zilikuwa kati ya nyimbo kuu zilizovuma katika taaluma yake. Alikuwa maarufu kwa mtindo wake wa Takeu staili.
Marejeo
- ↑ "Meet Tanzania music legend Mr Nice on his career downfall, family, health status, controversies". Maravi Post (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-03-26.
- ↑ "#TBT The Truth Behind What Really Happened To Mr Nice". Varcity (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2015-04-30.
- ↑ "Fagilia wote! Maina Kageni hooks up Mr Nice with three top producers". Mpasho (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-18.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mr Nice kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |