Nenda kwa yaliyomo

Asidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 11:35, 30 Agosti 2024 na Kimwali mmbaga (majadiliano | michango) (#WPWP #WPWPARK)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Asidi


Asidi ni kampaundi ya kikemia yenye uwezo wa kutoa protoni ya hidrojeni (H+) kwa kampaundi nyingine inayoitwa besi na tokeo la mmenyuko huo kuwa chumvi pamoja na maji.

Asidi za kila siku

[hariri | hariri chanzo]

Asidi iliyotumiwa na watu tangu karne nyingi ni siki; asidi ndani yake huitwa asidi asetia (CH3COOH).

Asidi nyingine inayotumiwa na watu wengi ni asidi salfuria (H2SO4) katika betri za magari.

Tabia za asidi

[hariri | hariri chanzo]
  • Asidi huathiri na hata kula metali na chokaa, pia mawe ya aina za chokaa kama marumaru.
  • Asidi ni pia hatari kwa nguo, ngozi na hasa macho. Hii ni sababu ya sheria kuhusu kutumia miwani ya kinga wakati wa kushughulika asidi.
  • Kuna asidi hafifu na asidi kali. Asidi hidrokloria (HCl) ni asidi kali, asidi asetia ni kali kiasi, na asidi kabonia (H2CO3) ni asidi hafifu.
  • Asidi inaweza kuchanganywa na maji. Athira yake inapungua kadiri ya kiwango cha maji.
  • Asidi nyingi hupatikana kama hali ya majimaji, lakini kuna pia asidi katika hali imara. Mifano yake ni vitamini C (asidi askobiki) au asidi sitriki.
  • Rangi ya buluu ya mimea au pia ya karatasi ya litmasi huwa nyekundu. Kwa sababu hiyo kipande kidogo cha karatasi ya litmasi ni njia ya kutambua mara moja kama kiowevu kina tabia ya kiasidi.
  • Besi hubatilisha tabia kali za asidi.
  • Ikiyeyushwa katika maji, asidi hupitisha umeme.
  • Asidi nyingi zina ladha chungu kama limau mdomoni.