Mr Nice
Mandhari
Mr Nice | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Lucas Mkenda |
Amezaliwa | Moshi, Tanzania |
Kazi yake |
Lucas Mkenda (maarufu kama Mr Nice[1]; alizaliwa Moshi, Tanzania, mwaka 1978) ni mwimbaji mkongwe wa Tanzania na mmoja wa waimbaji mashuhuri waliotawala muziki wa Afrika Mashariki mwanzoni mwa miaka ya 2000.[2]
Alianza kupata umaarufu mwaka 1999 baada ya kutoa albamu yake ya kwanza, Kidali Po, na kuelekea mwisho wa 2002, alitoa albamu yake ya pili, Rafiki, pia nyimbo zake kama; Kikulacho, Fagilia Wote[3] na Kuku Kapanda Baiskeli zilikuwa kati ya nyimbo kuu zilizovuma katika taaluma yake. Alikuwa maarufu kwa mtindo wake wa Takeu staili.
Maisha
Lucas Mkenda kwa sasa anaishi nchini Kenya na mkewe ambaye wana watoto wawili wa kike.
Mnamo 2021, mama wa Mr Nice aliyekuwa akiishi Moshi, Tanzania alifariki dunia.[4]
Diskografia
Albamu
- Kidali po
- Rafiki
Nyimbo
- Kikulacho
- Fagilia
- Nakuita
- Kidalipo
- Awe mama we
- Tabia gani
- Mama
- Tuvumiliane
- Kila mtu na demu wake
- Kuku kapanda baiskeli
- Mbona umeniacha
- King'asti[5]
Marejeo
- ↑ "Meet Tanzania music legend Mr Nice on his career downfall, family, health status, controversies". Maravi Post (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-03-26.
- ↑ "#TBT The Truth Behind What Really Happened To Mr Nice". Varcity (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-12-25. Iliwekwa mnamo 2015-04-30.
- ↑ "Fagilia wote! Maina Kageni hooks up Mr Nice with three top producers". Mpasho (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-18.
- ↑ "Mr Nice Mourns the loss of his mother". Standard Entertainment (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-26.
- ↑ "Watch: Mr Nice Tells Off Haters in Second Music Video After Hiatus". Nairobi Wire (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-02-12.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mr Nice kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |