Mshewa
Mshewa ni kata ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,471 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,154 [2] walioishi humo.
Kata ya Mshewa ina vijiji vya Marindi, Mshewa, Manka na Goma.
Mshewa ina ofisi ya kijiji, shule ya msingi, shamba la kilimo na jengo la kahawa linalomilikiwa na Vuaso Cooperative Union.
Pamoja na kanisa la mtaa KKKT usharika wa Marindi, Mshewa kuna Kanisa la Neno na kanisa la EAGT.
Watu maarufu
Mshewa aliishi Martin Shafuri, mchungaji mwenyeji wa kwanza eneo la Mbaga baada ya wamisionari wa kwanza wa Kilutheri. Mchungaji Shafuri wakati wa kustaafu alipewa kiti kimeandikwa "Ikaa si uheme". Alifariki mwaka 1976.
Karibu na nyumbani kwa Mchungaji Shafuri ametokea mchungaji wa pili hapo Mshewa, Elineema Mwakulala Mndeme ambaye alizaliwa tarehe 24 Aprili 1971. Alibarikiwa kuwa mchungaji tarehe 12 Septemba 1999.
Watu maarufu hapo Mshewa ni pamoja na familia za Simeon Mapande, Mwang'ombe, Mchungaji Martin Shafuri, Lukwaro Wiljohn Mwakulala, Sheshe, Timotheo Mnzava, mzee Fundi, mzee Kirito, mzee Hoseni (Kaloko), Mapande, Zuberi Mpanga, Rafaeli Semboja, mzee Ngwijo, Solomoni Chazuka na Enirisha ,mzee Omary mkose, preygod Liana mmbaga.
Marejeo
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Same DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-21.
Kata za Wilaya ya Same - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Bangalala | Bendera | Bombo | Bwambo | Chome | Gavao Sawene | Hedaru | Kalemawe | Kihurio | Kirangare | Kisima | Kisiwani | Lugulu | Mabilioni | Makanya | Maore | Mhezi | Mpinji | Mshewa | Msindo | Mtii | Mwembe | Myamba | Ndungu | Njoro | Ruvu | Same Mjini | Stesheni | Suji | Tae | Vudee | Vuje | Vumari | Vunta
|