Mbwa-kaya
Mbwa | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mbwa aina ya Labrador
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Mbwa (Canis lupus familiaris) ni mnyama anayefugwa na binadamu tangu muda mrefu. Kibiolojia anahesabiwa kati ya mamalia wanaokula nyama.
Watu na mbwa
Watu wametumia mbwa kulingana na utamaduni wao kwa njia mbalimbali kama mnyama wa kazi akilinda nyumba na mifugo au kubeba mzigo.
- Eskimo wa Aktiki wanatumia mbwa kwa usafiri wakivuta vitoroli vinavyoteleza juu ya barafu.
- Watu wa China Kusini, Korea na Vietnam wanakula nyama ya mbwa.
- Mara nyingi mbwa wanafugwa nyumbani kama wanyama wa kusindikiza watu tu wakitazamiwa kama marafiki.
- Kinyume chake katika utamaduni mwingine mbwa anaangaliwa kama najisi.
Mbwa wametumiwa kwa kazi nyingi.
- Wanalinda nyumba za watu.
- Wanaangalia na kulinda mifugo kwa mfano kondoo
- Wanaongoza watu vipofu,
- wanasaidi polisi,
- wanatafuta madawa ya kulevya au mabomu yaliyofichwa.
- Kiumbe cha kwanza kilichotoka duniani alikuwa mbwa jike Laika aliyerushwa angani tar. 3 Novemba 1957 kwa chombo cha angani cha kirusi Sputnik 2 akafa huko siku ileile.
Tabia
Kutokana na historia ndefu ya kufugwa na uteuzi wa kibinadamu kuna aina nyingi za mbwa wanaoonyesha miili tofautitofauti, Hata hivyo mbwa wote ni spishi moja tu na wote wanaweza kuzaa pamoja.
Mbwa huwa na uwezo mzuri wa kusikia na kunusa lakini hawaoni vizuri sana hasa rangi. Wanaweza kusikia sauti kwa umbali wa kilomita kadhaa.
Mbwa hufikia umri wa miaka 10 au zaidi.
Kiasili mbwa waliishi katika makundi yenye ufuatano wa vyeo. Mbwa mkuu huitwa "dume alfa". Mbwa wakiishi pamoja na binadamu wanawakubali kama mbwa wenye cheo cha juu.
-
Mkubwa na mdogo
-
Mbwa mlinzi akiangalia kondoo
-
Mbwa wakivuta gari
-
Mbwa wanaovuta kitelezi juu ya theluji
-
Kiongozi wa kipofu
-
Fanya fujo uone! Wasaidizi wa polisi (Uswidi)
-
Je wameficha madawa haramu?