Nenda kwa yaliyomo

Mbwa-kaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 01:52, 21 Januari 2010 na Jotterbot (majadiliano | michango) (roboti Badiliko: he:כלב הבית)
Mbwa
Mbwa aina ya Labrador
Mbwa aina ya Labrador
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama walao nyama)
Nusuoda: Caniformia
Familia: Canidae (Wanyama walio na mnasaba na mbwa)
Jenasi: Canis
Spishi: Canis lupus
Nususpishi: Canis lupus familiaris (Mbwa)
(Linnaeus, 1758)

Mbwa (Canis lupus familiaris) ni mnyama anayefugwa na binadamu tangu muda mrefu. Kibiolojia anahesabiwa kati ya mamalia wanaokula nyama.

Watu na mbwa

Watu wametumia mbwa kulingana na utamaduni wao kwa njia mbalimbali kama mnyama wa kazi akilinda nyumba na mifugo au kubeba mzigo.

  • Eskimo wa Aktiki wanatumia mbwa kwa usafiri wakivuta vitoroli vinavyoteleza juu ya barafu.
  • Watu wa China Kusini, Korea na Vietnam wanakula nyama ya mbwa.
  • Mara nyingi mbwa wanafugwa nyumbani kama wanyama wa kusindikiza watu tu wakitazamiwa kama marafiki.
  • Kinyume chake katika utamaduni mwingine mbwa anaangaliwa kama najisi.

Mbwa wametumiwa kwa kazi nyingi.

  • Wanalinda nyumba za watu.
  • Wanaangalia na kulinda mifugo kwa mfano kondoo
  • Wanaongoza watu vipofu,
  • wanasaidi polisi,
  • wanatafuta madawa ya kulevya au mabomu yaliyofichwa.
  • Kiumbe cha kwanza kilichotoka duniani alikuwa mbwa jike Laika aliyerushwa angani tar. 3 Novemba 1957 kwa chombo cha angani cha kirusi Sputnik 2 akafa huko siku ileile.

Tabia

Kutokana na historia ndefu ya kufugwa na uteuzi wa kibinadamu kuna aina nyingi za mbwa wanaoonyesha miili tofautitofauti, Hata hivyo mbwa wote ni spishi moja tu na wote wanaweza kuzaa pamoja.

Mbwa huwa na uwezo mzuri wa kusikia na kunusa lakini hawaoni vizuri sana hasa rangi. Wanaweza kusikia sauti kwa umbali wa kilomita kadhaa.

Mbwa hufikia umri wa miaka 10 au zaidi.

Kiasili mbwa waliishi katika makundi yenye ufuatano wa vyeo. Mbwa mkuu huitwa "dume alfa". Mbwa wakiishi pamoja na binadamu wanawakubali kama mbwa wenye cheo cha juu.

Ukweli

Ya mbwa Copper kutoka The Fox and the Hound akawa bora marafiki na mbweha aitwaye Tod. Hata hivyo, Copper ni mbwa uwindaji, na ana kuwinda rafiki yake.

Wikimedia Commons ina media kuhusu: