Nenda kwa yaliyomo

Dalmatia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 11:31, 8 Oktoba 2010 na Luckas-bot (majadiliano | michango) (roboti Nyongeza: an:Dalmacia)
Dalmatia (buluu-nyeusi) katika Kroatia - (buluu yote)

Dalmatia (Kikroatia: Dalmacija, Kiserbia: Далмација, Kiitalia Dalmazia) ni jina kwa nchi ya pwani la Adria katika kusini la Kroatia.

Inaanza kwenye kisiwa cha Rab upande wa kaskazini na kuendelea hadi mpaka wa Montenegro upande wa kusini. Upande wa bara mwisho wake ni mpaka wa Bosnia na Herzegovina.

Kihistoria hii ilikuwa eneo la miji-dola kwenye pwani iliyostawi kutokana na biashara ya baharini. Kati ya miji hii ni Split, Zadar, Šibenik na Dubrovnik.

Jina la "Dalmatia" limetokana na zamani za Roma ya Kale na hasa kabila la "Dalmatae" waliopigana na Waroma wa Kale. Leo hii wakazi walio wengi ni Wakroatia.