Nenda kwa yaliyomo

Leonardo da Vinci

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 21:53, 27 Novemba 2011 na JhsBot (majadiliano | michango) (Robot: af:Leonardo da Vinci is a featured article)
Leonardo da Vinci

Leonardo Da Vinci (15 Aprili 14522 Mei 1519) alikuwa mtu mwenye vipaji vingivingi kutoka nchini Italia. Kifupi, alikuwa mwanahisabati, mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi, mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji, msanifu majengo, mwanabotania, mwanamuziki, na mwandishi. Leonardo alikuwa mdadisi wa kila kitu asilia. Alitaka kujua kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa hodari sana katika masomo, kuunda na kutengeneza vitu vya aina mbalimbali tena vya kupendeza.[1]

Watu wengi hufikiria kwamba Leonardo alikuwa mmoja kati ya wachoraji bora wa muda wote. Watu wengi hufikiria kwamba alikuwa mtu aliyebarikiwa vipaji katika historia ya maisha.[2] Mwanahistoria wa sanaa Bi. Helen Gardner alisema kwamba hakuna mtu aliyewahi kuwa kama yeye kwa sababu alikuwa na shauku na vitu vingi sana: "...Akili yake na utu wake unaonekana kuwa zaidi ya mtu, ni mtu wa ajabu na tofauti".

Leonardo alizaliwa mjini Vinci ambapo ni mji mdogo ulio karibu na Florence nchini Italia. Alifunzwa kuwa msanii na mchongaji na mchoraji Verrocchio. Alitumia sehemu kubwa ya maisha yake akimtumikia tajiri mmoja maarufu wa Kiitalia. Katika miaka yake ya mwisho aliishi katika nyumba yake nzuri aliyopewa na Mfalme wa Ufaransa.

Leonardo aliweza kufanya vitu vya aina nyingi vya kijanja, lakini alikuwa maarufu sana kama mchoraji. Miongoni mwa picha zake mbili maarufu duniani ni pamoja na Mona Lisa na Last Supper. Amefanya michoro mingi sana. Mchoro unaojulikana sana ni Vitruvian Man. Unajulikana sana hata Homer Simpson na Garfield ambazo zilichorwa kwa mraba na mzunguko ili kuonekana kama mchoro. Leonardo siku zote alikuwa akifiria kugundua mambo mapya. Vitu vingi alivyogundua havikuwahi kufanywa. Hata hivyo, tunajua fikra zake, kwa sababu aliweka kwenye vijitabu na kuandika na kuvichora mara kwa mara. Baadhi ya nadharia alizofikiria ni pamoja na helicopta, kifaru, kikokotoo,roboti na vifaa vinavyogeuza nishati ya jua kuwa umeme.

Maisha

Utotoni mwake, 1452–1466

Mchoro uliojulikana awali wa Leonardo, Arno Valley, (1473) - Uffizi

Leonardo alizaliwa mnamo tar. 15 Aprili, 1452, mjini Tuscan mji wa kilima cha Vinci, katika mabonde ya Mto Arno. Babu yake, Ser Antonio, anajuvunia kwa kuweka kumbukumbu ya maelezo. Wazazi wa Leonardo walikuwa hawaja oana. Baba'ke alikuwa mwanasheria, Messer Piero Fruosino di Antonio da Vinci.[3][4] Mama'ke, Caterina, alikuwa muhudumu. Yawezekana alikuwa mtumwa kutoka Mashariki ya Kati.[5][6] Jina kamili la Leonardo lilikuwa "Leonardo di ser Piero da Vinci", ambalo lina manaa ya "Leonardo, mtoto wa Messer (Mister au Bwana) Piero kutoka Vinci".

Leonardo alitumia miaka yake mitano ya awali akiishi katika nyumba ya shamba na mama'ke. Halafu akaja kuishi mjini Vinci na baba'ke, mke wa baba'ke aliitwa Albiera, mabibi/mababu zake na wajomba zake, Francesco. Wakati Leonardo kakua, aliandika vitu viwili tu kuhusu maisha yake ya utotoni. Alikumbuka kwamba alivyokuwa amelala kwenye kitanda chake cha watoto nje ya nyumba yao ndege mkubwa alikuwa akipaa na kumzungukazunguka juu yake. Mikia yake ikawa inamfutafuta sura yake.[7] Kumbumbu nyingine muhimu ya Leonardo ilikuwa vipi aligungua pango milimani wakati anapeleleza. Alikuwa na hofu kubwa sana huenda kukawa na kiumbe cha ajabu kikubwa kimejificha mule ndani ya pango. Lakini pia alikuwa na hamu na shauku ya kujua nini kilichopo ndani mule.

Leonardo alianza kuchora tangu yungali bado kijana. Giorgio Vasari aliandika kuhusu maisha ya Leonardo kwa ufupi baada ya kifo chake. Ameelezea hadithi za kuvutia kibao kuhusu ujanja aliokuwa nao Leonardo. Anasema kwamba Leonardo alichora bamba la taarifa la mbao-mzunguko likiwa na picha ya mijoka inayotema moto. Messer Piero alichukua michoro ya mwanawe hadi Florence na kuiza kwa wauzaji wa bidhaa za kisanaa.[8]

The Baptism of Christ (1472–1475)—Uffizi, by Verrocchio and Leonardo

Kifo

Mwaka 1516 Leonardo alikwenda Amboise, Ufaransa, baada ya kupata mualiko kutoka kwa mfalme Francis wa kwanza na kati ya mizigo aliyosafiri nayo ulikuwemo mchoro maarufu wa Monalisa. Leonardo aliishi Amboise toka mwaka huo wa 1516 mpaka mwaka 1519, alifariki Mei 2 1519 mjini Amboise na kuzikwa St. Hubert akiwa na umri wa miaka 67, lakini taarifa za afya yake hazikuwa nzuri kwasababu Leonardo alipata ugonjwa wa kiharusi toka mwaka 1517 lakini taarifa za ugonjwa wake zikatolewa wiki chache kabla ya kifo chake.

Marejeo

  1. Gardner, Helen (1970), Art through the Ages, Harcourt, Brace and World
  2. Vasari, Boltraffio, Castiglione, "Anonimo" Gaddiano, Berensen, Taine, Fuseli, Rio, Bortolon, etc as quoted in della Chiesa, see Bibliography
  3. Vezzosi, Alessandro, Leonardo da Vinci: Renaissance Man
  4. Angela Ottino della Chiesa, The Complete Paintings of Leonardo da Vinci
  5. According to Alessandro Vezzosi, Head of the Leonardo Museum in Vinci, Piero may have owned a Middle Eastern slave called Caterina. A study of Leonardo's fingerprint suggests that he may have had Middle Eatern blood.Experts Reconstruct Leonardo Fingerprint" December 12, 2001
  6. Experts Reconstruct Leonardo Fingerprint, The Associated Press, iliwekwa mnamo 2007-12-14
  7. Bortolon, Liana (1967), The Life and Times of Leonardo, London: Paul Hamlyn
  8. Giorgio Vasari, Lives of the Artists, 1568; this edition Penguin Classics, trans. George Bull 1965, ISBN 0-14-044164-6
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Leonardo da Vinci kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA