Bhutan
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Nchi moja, taifa moja" | |||||
Wimbo wa taifa: Druk tsendhen | |||||
Mji mkuu | Thimphu | ||||
Mji mkubwa nchini | Thimphu | ||||
Lugha rasmi | Dzongkha | ||||
Serikali | Ufalme Jigme Khesar Namgyal Wangchuck Khandu Wangchuk | ||||
Formation Wangchuk Dynasty |
17 Desemba 1907 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
47,000 km² (ya 131) | ||||
Idadi ya watu - 2006 kadirio - 2006 sensa - Msongamano wa watu |
672,425 (ya 142) 672,425 46/km² (ya 149) | ||||
Fedha | Ngultrum (BTN )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
BTT (UTC+6:00) (haitumiki) (UTC+6:00) | ||||
Intaneti TLD | .bt | ||||
Kodi ya simu | +975
- |
Bhutan ni nchi ndogo ya Bara Hindi katika milima ya Himalaya. Imetawaliwa na mfalme Jigme Singye Wanchuck tangu 1972. Nchi imepakana na Uhindi na jimbo Tibet la China. Kuna wakazi lakhi nane takriban. Mji mkuu unaitwa Thimphu.
Jiografia
Bhutan ni nchi ya milima na zaidi ya 80% za eneo la Bhutan ziko juu ya kimo cha 2,000 m. Kusini tu kuna kanda nyembamba ya tambarare ya Duar. Watu walio wengi hukalia eneo milimani katiy a 2,000 hadi 3,000 m juu ya UB. Mpakana na China kuna milima ya juu ya Lunana. Kula Kangri ni mlima mkubwa mwenye kimo cha 7,553 m.
Zaidi ya theluthi mbili za nchi zimefunikwa na misitu.
Wakazi na Utamaduni
Wabhutan walio wengi huishi mlimani wako karibu kiutamaduni na kilugha na watu wa Tibet na Burma. Hawa hufuata dini ya Ubuddha.
Watu wa kusini wanafana zaidi na watu wa Nepal na hutumia lugha ya Kihindi-Kiulaya. Wanafuata dini ya Uhindu.
Bhutan inajitahidi kutunza utamaduni wake. Hadi 1974 watalii hawakuruhusiwa kutembelea nchi. Baadaye imewezekana lakini si rahisi kupata kibali.
Historia
Bhutan ilianzishwa 1644 na mmonaki Mbuddha Shabdrung Ngawang Namgyel. Nchi iliweza kutunza uhuru wake hadi leo. Lakini ililazimishwa kukubali ya kwamba maeneo katika kusini yalitwaliwa na Waingereza na kuunganishwa na Uhindi wa Kiingereza. Uingereza ilishughulika pia mawasiliano ya nje ya Bhutan. Uhusiano huu umeendelea na India kulingana na mkataba wa urafiki wa 8 Agosti 1949. Tar. 12 Februari 1971 Bhutan ikapokelewa kama nchi mwanachama wa UM.
Viungo vya nje
- (Kiingereza) Tovuti ya serikali
- (Kiingereza) The Bhutan Times (gazeti)
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bhutan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |