Nenda kwa yaliyomo

Bahari ya Kusini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 05:09, 23 Desemba 2011 na TjBot (majadiliano | michango) (r2.5.4) (roboti Nyongeza: as:দক্ষিণ মহাসাগৰ)
Bahari ya Kuini inayozunguka bara la Antaktiki
Ramani hii inaonyesha mabadiliko ya halijoto ya maji ya bahari za dunia katika mwendo wa mwaka. Inaonekana jinsi gani kanda la barafu linalozunguka pwani la Antaktika (chini kabisa, rangi ya kijivu) hupanuka na kurudi nyuma kila mwaka

Bahari ya Kusini (pia: Bahari ya Antaktiki) ni jina jipya katika jiografia. Linamaanisha maji yote kusini ya latitudo ya 60 yanayozunguka bara la Antaktiki.

Katika eneo hili maji ya Bahari ya Atlantiki, Bahari Hindi na Pasifiki hukutana na kuingiliana. Kwa muda mrefu wataalamu walihesabu eneo kama itengo vya bahari tatu kubwa lakini katika karne ya 20 wazo la kuitazama kama bahari ya pekee imesambaa.

Eneo lote ni kilomita za mraba 20,327,000 za maji. Linazunguka pwani la Antaktika lenye urefu wa kilomita 17,968 km. Kina kikubwa ni mnamo 5,805 mita.

Sehemu zake karibu na pwani hufunikwa na barafu inayokua wakati wa baridi. Katika miezi ya joto vipande vikubwa vya barafu huvunjika na kuelea katika maji kama siwa barafu ambako ni hatari kwa ajili ya meli lakini zinayeyuka polepüole kadri jinsi zinavyofika maji yasiyo baridi tena.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.