Fumbwe
Fumbwe | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Fumbwe ni ndege wadogo wa jenasi Vidua katika familia Viduidae ambao wanatokea Afrika tu. Spishi bila mkia mrefu na yenye rangi ya nili wanaitwa kinili pia. Wakati wa kuzaa madume wana rangi ya nyeusi na nyeupe na pengine rangi nyingine au rangi ya nili tu, na spishi kadhaa zina mkia mrefu. Lakini wakati wengine wana rangi za majike, kahawia na nyeupe, wenye michirizi miwili kwa utosi, na mkia wao una urefu wa kawaida. Hula mbegu za manyasi hasa lakini wadudu pia, kumbikumbi aghalabu.
Ndege hawa hawajengi tago lao lenyewe lakini huyataga mayai yao katika matago ya ndege wa familia Estrildidae (udusio wa kiota, Kiing. brood parasitism). Kila spishi inadusia spishi yake ya Estrildidae. Vinili wadusia mitolondo, mshigi tombo au mshigi kidari-machungwa, na fumbwe wengine wadusia tunguridi, tunguhina au mishigi mbalimbali. Kinyume na kekeo fumbwe hawaharibu mayai ya mwenye tago. Huyataga mayai 2-4 kwa kuzidi yaliyomo. Mayai ya fumbwe ni meupe kama yale ya mwenyeji lakini wakubwa zaidi. Ndani ya domo la makinda inafanana na ile ya makinda ya mwenyeji na dume anaiga wimbo wake.
Spishi
- Vidua camerunensis, Kinili wa Kameruni (Cameroon Indigobird)
- Vidau chalybeata, Kinili-kaya (Village Indigobird)
- Vidua codringtoni, Kinili Kijani (Zambezi au Green Indigobird)
- Vidua fischeri, Fumbwe Mkia-njano (Straw-tailed Whydah)
- Vidua funerea, Kinili Mweusi (Dusky au Variable Indigobird)
- Vidua hypocherina, Fumbwe Buluu (Steel-blue Whydah)
- Vidua interjecta, Fumbwe Mgutaji (Exclamatory Paradise Whydah)
- Vidua larvaticola, Kinili Barka (Barka Indigobird)
- Vidua macroura, Fumbwe Mkia-mwembamba (Pin-tailed Whydah)
- Vidua maryae, Kinili wa Jos (Jos Plateau Indigobird)
- Vidua nigeriae, Kinili wa Nijeria (Quailfinch Indigobird)
- Vidua obtusa, Fumbwe Mkia-mpana (Broad-tailed Paradise Whydah)
- Vidua orientalis, Fumbwe wa Saheli (Sahel Paradise Whydah)
- Vidua paradisaea, Fumbwe Mkia-mrefu (Long-tailed au Eastern Paradise Whydah)
- Vidua purpurascens, Kinili Miguu-myeupe (Purple Indigobird)
- Vidua raricola, Kinili wa Jambandu (Jambandu Indigobird)
- Vidua regia, Fumbwe Mfalme (Shaft-tailed Whydah)
- Vidua togoensis, Fumbwe wa Togo (Togo Paradise Whydah)
- Vidua wilsoni, Kinili wa Wilson (Wilson's Indigobird)
Picha
-
Kinili-kaya
-
Kinili mweusi
-
Fumbwe mgutaji
-
Fumbwe mkia-mwembamba
-
Fumbwe mkia-mpana
-
Kinili miguu-myeupe
-
Fumbwe wafalme