Nenda kwa yaliyomo

Pamba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.
Kwa matumizi mbalimbali ya neno hili angalia hapa


Pamba tayari kwa mavuno

Pamba ni nyuzi nyeupe na laini zinazotokana na tunda la mpamba (Gossypium sp.). Nyuzi hizi zinaonekana kama sufi na mipamba inalimwa kwa nyuzi hizi ambazo ni msingi wa kutengeneza kitambaa na nguo.

Ndani ya tunda nyuzi za pamba zinaunganishwa na punje za mbegu wa mmea. Kusudi yao ni kusambaza mbegu kwa sababu zinafanya kazi kama tanga zinashika nguvu ya upepo na kuwezesha mbegu kuelea hewani mbali kiasi.

Pamba yenyewe inapatikana kutoka spihi nyingi za gossypium zinazokua kiasili katika sehemu mbalimbali za dunia. Lakini karibu pamba yote inayolimwa kwa matumizi ya nguo imetokana na spishi nne za mipamba ambazo ni

  • Gossypium herbaceum L. (asili ya Asia)
  • Gossypium arboreum L. (asili ya Asia)
  • Gossypium hirsutum L. (asili ya Amerika)
  • Gossypium barbadense L. (asili ya Amerika).

Kitambaa cha pamba huwa na faida nyingi kuliko vitambaa vya sintetiki. Pamba inaweza kushika unyevu hadi asilimia 80% ya uzito wake hivyo kitambaa chake kinapendeza hasa katika mazingira ya joto kwa sababu mtu husumbuliwi sana na jasho.

Mipamba shambani
Fukusitunda (Anthonomus grandis) anakula mpamba na kutaga mayai ndani ya matunda yake na kuharibu mavuno
Mavuno ya kisasa kwa kutumia mashine inayovuna pamba na kuigandamiza kama mabloku makubwa kwa usafiri

Mavuno duniani 2004/2005

2004/2005 jumla ya tani 26.043.000 t za pamba zilivunwa duniani. Nchi zenye mavuno kubwa zilikuwa zifuatazo:

Nchi zenye mavuno makubwa ya pamba (2004/05)
 Rang  Nchi Mavuno (kwa t elfu) Asilimia ya mavuno ya dunia
   1 China    6.320 24,27 %
   2 USA    5.062 19,44 %
   3 Uhindi    4.080 15,67 %
   4 Pakistan    2.415 9,27 %
   5 Brasilia    1.250 4,80 %
   6 Usbekistan    1.134 4,36 %
   7 Afrika ya Magharibi1    1.040 3,99 %
   8 Uturuki    900 3,46 %
   9 Australia    613 2,35 %
   10 Ugiriki    390 1,50 %
   11 Syria    331 1,27 %
   12 Misri    291 1,12 %
   13 Turkmenistan    203 0,78 %
   14 Tajikistan    172 0,66 %
   15 Kazakhstan    148 0,57 %
    Wengine    1.694 6,51 %
    Dunia yote    26.043 100,00 %
(1) Afrika ya Magharibi inajumlisha Benin (152), Burkina Faso (257), Kamerun (105), Chad (85), Cote d'Ivoire (130), Mali (240) na Togo (71)
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pamba kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.