Nenda kwa yaliyomo

Ueleaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.
Nguvu ya ueleaji ndani ya kiowevu

Ueleaji ni nguvu ya usukumaji juu wa giligili (yaani kiowevu au gesi) kwa gimba ndani yake. Hutokana na tofauti ya kanieneo (shindikizo) ya giligili kwenye sehemu za chini na juu za gimba.

Kani ya ueleaji juu unalingana na uzito wa giligili iliyosukumwa kando na gimba ndani yake. Kani hii inasababisha gimba kuelea au hata kupaa juu.

Ueleaji ni muhimu kwa vyombo kama boti, meli, puto au ndegeputo.

Densiti

Kama gimba ndani ya giligili huwa na densiti sawa nayo linaelea tu; kama densiti yake ni kubwa linazama chini; kama densiti yake ni ndogo kushinda giligili litapanda juu kwa uso wa giligili.

Meli au boti inaelea kwa sababu jumla ya mjao wake ni nyepesi yaani densitiy a wastani ni ndogo kuliko maji. Hii ni kweli hata kama ni meli ya feleji na feleji ina densiti kubwa na kuwa nzito kushinda maji. Lakini ndani ya felejikuna nafasi kubwa ya hewa na ni wastani ya nafasi hii yote inayofanya meli kwa jumla kuwa na densiti ndogo kuliko maji hivyo inaelea.

F ni alama ya kani ya ueleaji; ni mjao (=volume) ya giligili iliyosukumwa kando na gimba; ni densiti yake.

Hali hii ilitambuliwa na mtaalamu Archimedes wa Ugiriki ya Kale na kuelezwa naye katika kanuni yake.

Viungo vya Nje