Nenda kwa yaliyomo

Diamond Platnumz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Diamond Platnumz

Maelezo ya awali
Amezaliwa Oktoba 2 1989 (1989-10-02) (umri 35)
Asili yake Kigoma Tanzania
Kazi yake Mwimbaji, Mtunzi
Aina ya sauti "Tenor" ya tatu
Miaka ya kazi 2010–mpaka sasa
Studio Wasafi Records

Nasibu Abdul Juma Issaack (maarufu kwa jina la kisanii kama Diamond Platnumz; majina mengine ya kisanii ni kama Chibu, Simba, Nasibu kichwa, Simba la masimba ama Dangote; alizaliwa Dar es Salaam, Tanzania, 2 Oktoba 1989) ni mwimbaji wa nyimbo za Bongo Flava na Mtumbuizaji kutoka Tanzania. Ni mwimbaji na mtunzi wa muziki wa Kitanzania ambaye ana uwezo mkubwa wa kiushindani, hivyo ana mashabiki wengi ndani na nje ya Tanzania. Inasemekana kuwa ndiye msanii wa Afrika Mashariki na Kati anayependwa na kupambwa na watu wengi zaidi kwa sasa.

Amekuwa na nyimbo nyingi zikiwa ni pamoja na "Number One" ambao aliimba na mwimbaji tokea nchini Nigeria maarufu kama Davido. Na mwingine ni Komasava (Comment Ça Va)-Remix aliowashirikisha wasanii kutoka Afrika ya Kusini, Khalil Harrison na Chley Nkosi pamoja na Jason Derulo kutoka Marekani[1]

Nasibu Juma ameshinda tuzo nyingi zinazoandaliwa "Channel O" na "Hip-hop Music Awards". Pia amefanya kazi katika Mkutano Mkuu wa Ndugu Afrika Mei 2012.

Inaaminika kuwa ni msanii anayelipwa kutumbuiza kwenye tamasha kutoka nchini Tanzania kwa bei ya juu kabisa na makampuni ya simu ya mkononi mwaka 2013, pamoja na kuwa kati ya wasanii wanaopata kipato cha juu zaidi katika sekta ya muziki Afrika Mashariki.

Aidha msanii huyu amekuwa hasimu mkubwa wa kimuziki na msanii Ali Kiba ijapokuwa wote wawili wamekuwa wakikataa uhasama baina yao wakihamishia tuhuma hizo kwa mashabiki.

Nchi za wasanii ambao Diamond Platnumz ametoa nyimbo nao.

Mzaliwa wa Dar es Salaam mwenye asili ya Kigoma, Diamond ni Mwislamu.

Mwaka 2010, alikubali chama tawala cha Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mgombea wake wa urais, Jakaya Kikwete. Pia aliandika remix ya wimbo wake mmoja.

Nasibu Juma anasimamiwa na Babu Tale pamoja na Said Fella kutoka sekta ya muziki wa Tanzania. Anasemekana kuwa mwanamuziki tajiri zaidi katika Afrika Mashariki. Mnamo Februari 2018 alizindua Wasafi Tv na redio yake mpya nchini Tanzania. Ni mwanamuziki wa pili baada ya Youssou Ndour wa Senegal kumiliki TV na kituo cha redio barani Afrika.

Nasibu Juma (Diamond Platnumz) alia achia albumu yake ya kwanza mnamo mwaka 2010, iliyo kwenda kwa jina la Kamwambie yenye jumla ya nyimbo 12. Baada ya hapo akaachia album ya pili mnamo mwaka 2012 iliyo itwa Lala Salama ambayo ilikua na nyimbo 10.

Pia alizindua albamu yake ya tatu, A Boy From Tandale huko Nairobi katika maandamano ya 2018.

Ana watoto wanne ambao ni Dylan Abdul (aliyezaa na Hamisa Mobeto japo kumekuwa na sintofahamu juu ya Diamond kuwa baba wa mtoto huyo), Lattifah na Nillan Nasibu Abdul (aliyezaa na Zari Hassan, mfanyabiashara wa Uganda) pamoja na Nasibu Abdul Nasibu (aliyemzaa na mtangazaji na mwanamuziki Natasha Donna toka Kenya). Pia ni rafiki wa wengi.

Msikiti Mjini Kigoma

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Disemba 2019 Naseeb Abdul Juma alizindua rasmi msikiti mjini Kigoma aliyogharamia na kuikabidhi kwa viongozi Waislamu wa mji huo[2]. Shehe Ponda Issa Ponda alisema hakubali msikiti huo kwa sababu anaamini pesa za ujenzi huo ni haramu, akikosoa viongozi wenzake wa Kigoma waliokubali zawadi ya mwimbaji.[3]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Diamond ametoa albamu rasmi tarehe 14 Machi 2018, A Boy From Tandale, japo mnamo mwaka 2012 alitoa albamu isiyo rasmi ya "Nitarejea".

Pia ametoa Extended play list (EP) inayoitwa First Of All (FOA) 11 Machi 2022, ambayo ilipata watazamaji wengi ndani ya muda mfupi.

Tuzo na uteuzi [4]

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 3 Mei 2014, Diamond Platnumz aliweka rekodi mpya kwenye Tuzo za Muziki Tanzania kwa kushinda tuzo 7, ikiwa ni pamoja na Mwandishi Bora wa Kiume, Msanii Bora wa Kiume, Mwandishi wa Maneno Bora na Msanii Bora wa Kiume wa Mwaka. Rekodi ya awali iliwekwa na 20%, msanii wa kurekodi ambaye alitembea mbali na tuzo 5 katika Tuzo za Muziki Tanzania. Kwa kufikia mafanikio, Nasibu Juma aliweka rekodi ya kushinda tuzo 3 katika tuzo za muziki za Tanzania. Kwa mwaka 2024, Diamond Platnumz hajashinda tuzo yoyote kubwa. Hata hivyo, alitumbuiza kwenye Tuzo za CAF 2024 zilizofanyika nchini Morocco. Pia, aliteuliwa katika Tuzo za Muziki za Tanzania (Tanzania Music Awards) katika kipengele cha Wimbo Bora wa Mwaka kupitia wimbo wake "Yatapita". Pia mwaka 2024 mwezi desemba alifanya kazi na wasanii mbalimbali akiwemo Simi kutokea Nigeria na Fally Ipupa kutokea Congo. Katika kutangaza biashara ya mtandao wa Airtel "smarter data"

Tuzo za Muziki

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Mteule / kazi Tuzo Matokeo Ref
2016 Kidogo Video ya Afrika ya Mwaka Alishinda
2016 Kidogo Video bora ya Afrika ya Combo Alishinda
2016 Kidogo Utendaji Bora wa Afrika Alichaguliwa
2016 Kidogo Video Bora ya Kiume ya Afrika Alishinda
2016 Kidogo Video Bora ya Afrika Mashariki Alichaguliwa

| 2023 || MTV EMA|| Africa Global Act || Alishinda || |}

  1. Komasava (Comment Ça Va), 2024-05-02, iliwekwa mnamo 2024-07-28
  2. Diamond Platinumz launches his mosque in Tanzania Ilihifadhiwa 18 Februari 2020 kwenye Wayback Machine., tovuti ya theweekpost.com, iliangaliwa Februari 2020.
  3. Sheikh rejects Diamond’s Kigoma mosque calling it ‘haram’, gazeti The Citizen, tar 11-01-2020, iliangaliwa Februri 2020
  4. Orodha hii haijakamilika; unaweza kusaidia kwa kuipanua.


Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Diamond Platnumz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.