Yuda Tadei
Mitume wa Yesu |
---|
|
Yuda Tadei ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambalo Injili zinajitahidi kumtofautisha na Yuda Iskarioti, msaliti wa Yesu.
Habari zake za hakika zinategemea Agano Jipya ambamo anatajwa katika orodha ya Thenashara ambao waliteuliwa na Yesu Kristo kama msingi wa taifa jipya la Mungu wakatumwa naye kuhubiri na kuponya.
Injili ya Yohane tu inaripoti neno lake moja, katika simulizi la karamu ya mwisho, alipomuuliza Yesu imekuwaje atajifunua kwao lakini si kwa ulimwengu (14:22). Yesu alimjibu kwamba yeyote anayempenda atashika neno lake, na Baba atampenda na kufanya maskani yake kwake pamoja na Mwana[1].
Anafikiriwa na wengi kuwa mwandishi wa Waraka wa Yuda, lakini hakuna hakika kwa sababu jina hilo la babu wa Wayahudi wote lilikuwa la kawaida mno.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Oktoba pamoja na Mtume Simoni Mkananayo [2][3].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Catherine Fournier, Saint Simon and Saint Jude
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yuda Tadei kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |