Rasilmali
Mandhari
(Elekezwa kutoka Rasilimali)
Rasilmali (kutoka Kar. رأس المال ra's almal), pia mtaji, ni dhana muhimu katika elimu ya uchumi.
Inataja moja kati ya vyombo vya uzalishaji kufuatana na elimu ya uchumi pamoja na ardhi, kazi na elimu.
Rasilmali huwa na tabia zifuatazo
- ni tokeo la kazi ya kibinadamu (tofauti na ardhi ya yaliyomo yake kama malighafi)
- inatumiwa katika uzalishaji wa vitu
Rasilmali inataja vitu kama zana, mashine, majengo n.k. vilivyowahi kutengenezwa katika uzalishaji wa awali na sasa vinatumiwa kuzalisha vitu vingine.
Rasilmali ni pia pesa zinazopatikana kwa kutunza na kupanusha vyombo vya uzalishaji.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |