Mwinda
Mandhari
(Elekezwa kutoka Wala nyama)
Mwinda[1] (kwa Kiingereza: predator) kwa lugha ya biolojia ni mnyama ambaye anatumia wanyama wengine kama windo kwa kusudi la chakula; kwa kawaida kiumbehai cha windo kinauawa[2].
Kwa mfano buibui anayekamata na kula nzi ni mwinda. Vilevile kundi la simba wanaomwua na kula pundamilia ni wawinda. Nzi au pundamilia katika mifano hii ni windo.
Wanyama wawinda wengi ni walanyama, wengine walavyote, lakini si walanyama wote ni wawinda, kwa kuwa baadhi wanakula mabaki ya mizoga.
Kuna pia mimea michache ambayo inapata chakula kwa kuwinda wadudu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Mwinda ni msamiati wa Kiswahili wa Kamusi sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia (TUKI 2012) kwa "predator"
- ↑ Robert J. Taylor: Predation (= Population and Community Biology.). Chapman & Hall, London 1984, ISBN 0-412-25060-8.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwinda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |