Nenda kwa yaliyomo

Kreta ya volkeno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.
Kasoko ya volkeno Mount St. Helens (Marekani) baada ya mlipuko wa 1980 - sehemu ya ukingo umepotea

Kreta ya volkeno (kutoka gir./ing. crater, pia: kasoko ) ni shimo kubwa katika mlima wa volkeno.

Zaha na gesi za joto zinapotoka ardhini kuwa volkeno husababisha kutokea kwa kreta. Milima ya volkeno huwa na kasoko kwenye kelele mara nyingi pia na kasoko kando.

Kretaza volkeno inayolala au iliyozimika mara nyingi hujaa maji kuwa "ziwa la kreta".

Shimo linaweza kuonekana kubwa zaidi kama volkeno imeporomoka ndani yake yenyewe halafu huitwa "kaldera".