Air Force (viatu)
Mandhari
Air Force ni mfululizo wa matoleo ya viatu vya riadha kutoka katika kampuni ya Nike Inc.
Kampuni hiyo imetoa viatu aina ya Air force kwa kuanza na Air Force 1 na kuendelea na mwendelezo wa viatu vingine kama Air Force 2, Air Force 3, Air Force STS, Air Force 5, Air Force XXV na Air Force 09. Kiatu cha Air force 1 kiliundwa na mbunifu aliyeitwa Bruce Kilgore, na ndio kilikua kiatu cha kwanza cha mpira wa kikapu kutumia teknolojia ya kampuni ya Nike. Kiatu hicho kina matoleo ya Air force 1 low (cha chini), Air force 1 mid (cha kati) na Air force 1 high(cha juu) lakini katika matoleo hayo yote Air force 1 low(cha chini) ndicho kinachovaliwa sana na watu Duniani.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Air Force (viatu) kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |