Nenda kwa yaliyomo

Atlas (milima)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
milima ya atlas

Kwa matumizi tofauti ya jina hili tazama Atlas (maana)

Safu za milima ya Atlas.

Milima ya Atlas (kwa Kiberber: Idurar n Watlas; kwa Kiarabu: جبال الأطلس‎, jibaal al-atlas) ni safu ya milima kunjamano katika Afrika ya kaskazini-magharibi. Ina urefu wa takriban kilomita 2,400 kuanzia Moroko kwa kuvukia Algeria hadi Tunisia. Milima ya Atlas hutenganisha pwani ya Atlantiki na Mediteranea kutoka jangwa la Sahara.

Mwinuko wa juu ni Jebel Toubkal nchini Moroko inayofikia mita 4,167 juu ya UB.

Wakazi wa milima hii ni hasa makabila ya Waberber.

Jina la milima hii linatokana na mmoja wa miungu ya Ugiriki ya Kale, Atlas.

Atlas ni milima kunjamano yaani tokeo la kugongana kwa mabamba ya gandunia ya Afrika na Ulaya kulikosababisha kukunjwa kwa uso wa ardhi na kutokea kwa safu za milima hii. Mchakato huu ulitokea mara mbili. Mara ya kwanza takriban miaka milioni 300 iliyopita, wakati bamba la Amerika Kaskazini liligongana na bamba la Afrika na tokeo lake ni safu ya Antiatlas katika Moroko ya kusini. Lakini sehemu kubwa ya Atlas ilitokea kutokana na mgongano wa mabamba ya Afrika na Ulaya katika kipindi cha miaka milioni 65 - 2 iliyopita.[1][2]

Kutokana na historia hii kuna hatari ya mtetemeko wa ardhi katika eneo la Atlas na miji kadhaa iliwahi kuharibiwa.

Jina la Atlas linatokana na mhusika Atlas kwenye mitholojia ya Ugiriki ya Kale. Katika hadithi za Wagiriki huyu alikuwa mungu mmojawapo aliyepaswa kubeba anga kwa mabega yake. Hivyo makazi yake yaliaminiwa kuwa katika milima hiyo mirefu iliyo karibu na anga.[3]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. UAB.es Ilihifadhiwa 17 Machi 2009 kwenye Wayback Machine. Potential field modelling of the Atlas lithosphere
  2. UAB.es Ilihifadhiwa 19 Machi 2009 kwenye Wayback Machine. Crustal structure under the central High Atlas Mountains (Morocco) from geological and gravity data, P. Ayarza, et al., 2005, Tectonophysics, 400, 67-84
  3. Atlas Mountains, makala katika Enyclopedia Britannica 1911, kupitia archive.org
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Atlas (milima) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.