Bangi nchini Tanzania
Bangi nchini Tanzania ni marufuku: kuuza, kulima au kukutwa na bangi [1] kama si kwa ajili ya tiba na utafiti [2], lakini inabaki kuwa dawa ya kawaida na hutumiwa kwa matumizi tofauti, kama utumiaji wa ndani na kuuzwa nje ya nchi. Tanzania ni mojawapo ya nchi barani Afrika ambayo inazalisha bangi kwa wingi. [3]
Kilimo
[hariri | hariri chanzo]Watu wanapanda bangi kwa njia isiyo halali, wanadai kwamba wanapata faida kubwa kushinda mazao mengine.
Nchini Tanzania mbangi hupandwa katika ukanda wa pwani (Tanga), ukanda wa kaskazini (Arusha, Manyara na Kilimanjaro), nyanda za juu za kusini (mkoa wa Iringa) na kanda ya ziwa (Shinyanga na Mara) [4].
Bangi inazalishwa maeneo ya vijijini. Inachukua miezi minne hadi mitano kwa bangi kukomaa ikilinganishwa na mazao mengine kama mahindi.
Uingizaji kutoka nje
[hariri | hariri chanzo]Bangi nyingine huingizwa kutoka nje ya nchi na kiingilio kikuu ni uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, uwanja wa ndege wa Kilimanjaro International Airport (KIA) na bandari ya Dar es Salaam na ya Zanzibar na uwanja mdogo wa ndege kama Tanga na Mwanza .
Matumizi
[hariri | hariri chanzo]Bangi hutumiwa kama dawa vijijini, hutumika kuponya maradhi kama maumivu ya sikio, homa na malaria.
Matawi ya mbangi hutumiwa kutengeneza na kuandaa mboga kwa chakula katika maeneo ya vijijini [5].
Utekelezaji wa sheria
[hariri | hariri chanzo]Serikali iliharibu baadhi ya mashamba na kuwaadhibu watu ambao walikuwa wakilima. Watu ambao wanakutwa na bangi au wanakutwa wakitumia bangi wanakamatwa na kufungwa kwa miaka mitano pamoja na adhabu ya ziada[6].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ DRUG CONTROL AND ENFORCEMENT ACT. 2015.
- ↑ https://www.thecitizen.co.tz/news/No-investor-has-shown-interest-to-cultivate-marijuana-/1840340-5574734-td1pe3/index.html
- ↑ "CANNABIS IN AFRICA" (PDF). Iliwekwa mnamo 14 Agosti 2017.
{{cite journal}}
: Cite journal requires|journal=
(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "cannabis in Tanzania". 2013-07-25.
- ↑ "Section 3, UNITED REPUBLIC OF TANZANIA" (PDF). Iliwekwa mnamo 14 Agosti 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ https://www.thecitizen.co.tz/news/No-investor-has-shown-interest-to-cultivate-marijuana-/1840340-5574734-td1pe3/index.html
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bangi nchini Tanzania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |