Nenda kwa yaliyomo

Bessie Head

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bessie Emery Head (6 Julai 1937 - 17 Aprili 1986) hutazamwa kama mwandishi muhimu zaidi wa nchi ya Botswana. Alizaliwa katika eneo la Pietermaritzburg, Afrika Kusini, mwana wa mwanamke tajiri mweupe wa Afrika Kusini na mtumishi mweusi wakati ambapo uhusiano kati ya watu wa rangi tofauti ulikuwa kinyume cha sheria. Mamake alikuwa na ugonjwa wa kiakili; matukio yenyewe si hakika lakini kutokana na taarifa chache za Bessie Head, ambazo hudokezwa kana kwamba zimetoka katika kitabu alichoandika kuhusu maisha yake, mara nyingi huwa zimetungwa.

Maisha ya kitaaluma

[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa mwalimu, halafu mwanahabari wa jarida la Drum katika miaka ya 1950 na '60.

Kuhamia Botswana

[hariri | hariri chanzo]

Alihamia Botswana, ambayo wakati huo ilikuwa ikiitwa Eneo la Kikoloni la Bechuanaland) mnamo mwaka wa 1964 kama mkimbizi, baada ya kujihusisha na siasa za Kipaniafrikani. Ilichukua miaka 15 klabla ya Head kupewa uraia nchini Botswana.

Bessie Head aliishi katika eneo la Serowe, ambalo lilikuwa kijiji kikubwa zaidi cha Botswana (yaani makazi ya kitamaduni ikitofautishwa na makazi ya kilowezi). Eneo la Serowe lilikuwa maarufu kwa umuhimu wake wa kihistoria, kama makao makuu ya kabila la Kibamangwato, na kwa shule la jaribio la Swaneng la Patrick van Rensburg. Chifu wa Kibamangwato aliyeng’olewa mamlakani Seretse Khama, baada ya miaka michache angekuja kuwa rais wa Botswana huru.

Uandishi

[hariri | hariri chanzo]

Kazi nyingi muhimu za Bessie Head zina muktadha katika eneo la Serowe, hasa riwaya tati When Rain Clouds Gather(Wakati Mawingu ya Mvua Yanapokusanyika), Maru, na A Question of Power(Swali la Nguvu). Mojawapo ya maandiko yake mazuri zaidi ni When Rain Clouds Gather (Wakati Mawingu ya Mvua Yanapokusanyika) ambapo anaandika kuhusu kijana mmoja mwenye shida nyingi anayeitwa Makhaya ambaye anatoroka katika pahali pake pa kuzaliwa, Afrika Kusini, kuwa mkimbizi katika kijiji kidogo cha Golema Mmidi, nchini Botswana. Katika kijiji hicho anakumbwa na changamoto nyingi. Moja ambayo ni kuwa Chief Matenge hamtaki katika kijiji hicho. Anakutana na mwanaume mweupe anayeitwa Gilbert na anaanza safari mpya kuelekea kusikojulikana. Pia alichapisha hadithi nyingi fupi, ikiwemo mkusanyiko wa hadithi The Collector of Treasures (Mkusanyaji wa Vitu vya Thamani). Pia alichapisha kitabu kuhusu historia ya Serowe, kijiji alichochagua kufanya kiwe makazi yake - Serowe: Kijiji cha Upepo wa Mvua. Riwaya yake ya mwisho ilikuwa na muktadha wa Botswana ya karne ya ishirini - A Bewitched Crossroad. (Barabara Zinazopitana za Kurogwa)

Maandiko ya Bessie Head, yaliyosisitiza thamani ya maisha ya kawaida na watu wa kawaida, iliwiana zaidi na mwenendo wa awali wa uandishi wa Kiafrika kinyume na uandishi wa leo ambapo waandishi wanataja taarifa za kisiasa waziwazi. Hata hivyo vitabu vyake vimedumu. Dhana za kidni zinaonekana bayana, wakati mwingine. Kama katika kitabu cha A Question of Power (Swali la Nguvu). Ni muhimu kutilia maanani kuwa Bessie Head mwanzoni alilelewa katika maisha ya Ukristo lakini mwishowe alifuata Uhindi (kupitia jamii ya Afrika Kusini ya Kihindi). Hata hivyo mtazamo wake wa Dunia ni mgumu kuelezea.

Kazi yake mingi ya uandishi ilifanyika alipokuwa uhamishoni nchini Boswana, isipokuwa riwaya yake ya mapema ya The Cardinals (Makasisi) (iliyochapishwa baada ya kifo chake), iliyoandsikwa kabla ya yeye kuhamia Afrika Kusini.

Kwa njia Fulani, Bessie Head alibaki akiwa ametengwa katika nchi aliyohamia, na kuna watu wanaotazama kana kwamba aliipenda na kuichukia nchi hiyo kwa wakati mmoja. Wakati mwingine aliathirika na shida za kiakili na wakati mmoja aliweka tangazo hatharani akitangaza madai ya kutisha kuhusu aliyekuwa rais Seretse Khama, ambayo ilimfanya akae kwa kipindi kifupi katika Hospitali ya Watu Wenye Ugonjwa wa Kiakili ya Lobatse. A Question of Power (Swali la Nguvu) ina msingi wake katika baadhi ya matukio haya.

Kifo chake mnamo mwaka wa 1986 (akiwa na umri wa miaka 49) kutokana na ugonjwa wa maini kilifanyika wakati alipokuwa ameanza kupata umaarufu na alipokuwa ameanza kuaga maisha ya umaskini.

Ya ziada

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwezi Julai mwaka wa 2007 makataba katika mji wa Pietermaritzburg yalipewa jina la Maktaba ya Bessie Head ili kumkumbuka.

Bibliography

[hariri | hariri chanzo]
  • When Rain Clouds Gather (Wakati Mawingu ya Mvua Yanapokusanyika) (1968)
  • Maru (1971)
  • A Question of Power (Swali la Nguvu) (1974)
  • Looking for a Rain God (Kumtafuta Mungu wa Mvua) (1977)
  • The Collector of Treasures and Other Botswana Village Tales (Mkusanyaji wa Vitu vya Thamani na Hadithi Zingine za Vijiji vywa Botswana) (1977)
  • Serowe: Village of the Rain Wind (Serowe:Kijiji cha Upepo wa Mvua) (1981)
  • A Bewitched Crossroad (Barabara yenye Njia Mbili iliyorogwa) (1984)
  • A Woman Alone: Autobiographical Writings (Mwanamke Peke Yake: Maadiko Kuhusu Maisha Yake) (1990)
  • A Gesture of Belonging: Letters from Bessie Head, 1965-1979 (Ishara ya Kuwa na Makao:Barua kutoka Bessie Head) (1991)
  • The Cardinals (Makasisi) (1993)
  • 2003 - Tuzo la Dhahabu la Ikhamanga kwa mchango wake wa kujitolea kuendeleza fasihi na mchango wa mabadiliko ya kijamii, uhuru na amani.[1]

References

[hariri | hariri chanzo]
  • Microsoft Encarta 98 Encyclopedia, 1993-97
  • Ibrahim, Huma. Bessie Head: Subversive Identities in Exile. (1996) Charlottesville: University Press of Virginia. ISBN 0-8139-1685-2
  • Eilersen, Gillian Stead. Bessie Head: Thunder Behind Her Ears - Her Life and Writings (Studies in African Literature). (1995) Cape Town: James Currey, ISBN 0-85255-535-0; (1996) London: Heinemann
  • Kate Bissell, http://www.english.emory.edu/Bahri/Head.html Ilihifadhiwa 9 Julai 2011 kwenye Wayback Machine., 16 Januari 2007.
  • Walker, Alice. "The Temple of My Familiar".

Citation

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Profile of Bessie Head", S A National Orders. Retrieved on 2007-04-26. Archived from the original on 2007-09-27. 
[hariri | hariri chanzo]