Nenda kwa yaliyomo

Chekecha Cheketua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Chekecha Cheketua”
“Chekecha Cheketua” cover
Kava ya Chekecha Cheketua
Single ya Ali Kiba
Imetolewa 29 Juni, 2015
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2015
Aina Pop, Bongo Flava
Urefu 3:30
Studio RockStar4000
Mtunzi Ali Kiba
Mtayarishaji Abby Daddy
Mwenendo wa single za Ali Kiba
"Mwana"
(2014)
"Chekecha Cheketua"
(2015)
"Nagharamia"
2015

"Chekecha Cheketua" ni jina la wimbo uliotoka 29 Juni 2015 wa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Ali Kiba. Wimbo umetayarishwa na Abby Daddy ukiwa wimbo wa pili kutolewa tangu kusimama kutoa kazi za kujitegemea miaka mitatu iliyopita. Video ya wimbo huu imeongozwa na Meji Alabi ambaye Kiba anamsifia kwa kusema anamuelewa sana kupita maelezo. Huu ulikuwa wimbo wa kwanza kufanya kazi na Meji ukafuatiwa na Aje kisha Aje Remix. Vilevile ni video ya pili kufanyiwa nchini Afrika Kusini. Hadi wimbo huu kutoka, Kiba bado ameweza kushikilia misingi ya Bongo Flava bila kutia vionjo vya nyimbo au uigizaji wa nyimbo za Afrika Magharibi. Wakati sehemu kubwa ya wasanii wa Tanzania wamekuwa wakiangukia mikononi mwa muundo wa muziki wa Nigeria na Ghana.[1]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Wakati wasanii wengi kwa sasa wakiiga vibwagizo vya Nigeria JamiiForum mnamo 27 Februari, 2015. Miezi minne kabla ya wimbo kutoka.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]