Chiapas
Mandhari
Chiapas (jina rasmi: Estado Libre y Soberano de Chiapas; Kiswahili: dola huru la kujitawala la Chiapas) ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko. Ni jimbo kwenye ncha ya kusini ya
nchi. Mji mkuu na mji mkubwa ni Tuxtla Gutiérrez.
Imepakana na Oaxaca, Tabasco, Veracruz na nchi ya Guatemala. Kunako mwaka wa 2005, idadi ya wakazi ilikuwa 4,293,459. Eneo la jimbo ni 74,211 km².
Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi. Mazao ya soko ni kahawa, asali na miwa. Kwa jumla eneo halikuendelea sana na wakazi ni kati ya watu maskini zaidi wa Meksiko.
Gavana wa jimbo ni Juan José Sabines Guerrero.
Lugha ni Kihispania na Kimaya.
Miji Mikubwa
[hariri | hariri chanzo]- Tuxtla Gutiérrez (503,320)
- Tapachula (282,420)
- San Cristóbal de las Casas (142,364)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kihispania) Estado de Chiapas Sitio oficial Ilihifadhiwa 19 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mexiko bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Chiapas kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |