Nenda kwa yaliyomo

Faro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Faro (pia: Faron au Burgundofaro; 596 - 670 hivi) alikuwa askofu wa Meaux nchini Ufaransa kwa walau miaka 30 akilikirimu Kanisa mali nyingi, na kuanzisha parokia na kutegemeza monasteri mbalimbali.[1].

Kabla ya hapo alikuwa akifanya kazi katika ikulu ya wafalme Theodoberti II, Theodoriko na Klotari II, lakini dada yake, Fara alimfanya atamani kumtumikia Mungu kikamilifu hata akamhimiza mke wake kujiunga na utawa ili yeye aingie upadri.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni 28 Oktoba[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/75485
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.