Nenda kwa yaliyomo

Harmonize

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Harmonize
Msanii wa muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Rajab Abdul Kahali
Pia anajulikana kama Harmonize
Asili yake Mtwara,Tanzania
Aina ya muziki Bongo Flava,Afro Pop
Kazi yake Mwimbaji-mtunzi, mtayarishaji wa rekodi
Ala Piano, sauti
Miaka ya kazi 2011–mpaka sasa
Studio Konde Music Worldwide
Ame/Wameshirikiana na Rayvanny, Diamond Platnumz
Tovuti Tovuti Halisi


Harmonize (kwa jina lake halisi Rajab Abdul Kahali; mara kadhaa hujiita "Konde Boy"; amezaliwa Chitoholi, mkoa wa Mtwara ni mwimbaji na mtunzi wa muziki kutoka Tanzania.

Alianza kuvuma kwa kibao chake cha kwanza "Aiyola" (2015), Bado (2016), Matatizo (2016) na baadaye akatoa nyimbo na msanii mwenzie kutoka lebo moja ya WCB (Wasafi Classic Baby) ambaye ni Diamond Platnumz.

Aliamua kuhama WCB na kuanzisha lebo yake Konde Music Worldwide [1].

Kwa ngwaru ni wimbo ambao ulibamba karibia maeneo yote ya Afrika ya Mashariki akatoa kibao kingine kiitwacho inama nyimbo ambayo aliimba na msanii kutoka nje ya Tanzania ambaye anaitwa Burna na Diamond Platnumz alikuwepo kwenye huo wimbo. Sasa hivi anatamba na kibao kiitwacho Never Give Up, wimbo ambao unaelezea historia ya maisha yake kuanzia alivyo kuwa na maisha magumu sana. Harmonize anasimamiwa na Joel Joseph au kwa jina lingine Mr Puaz. Kwa sasa msanii huyu yuko peke yake baada ya kujitoa WCB pia amekuwa akitoa ngoma kama vile uno ambayo imepata umaarufu mkubwa na kuwa gumzo yani number one on trending. Pia kwa sasa ameachia kazi yake ya pili iitayo kushoto kulia ambayo amesikika akimtaja Diamond ambapo ni kwa mara ya pili.

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Harmonize ana asili ya Mtwara. Alisoma katika shule ya sekondari Mkundi iliyopo mjini Mtwara. Baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari, Harmonize alielekea Dar es Salaam ambako alijipatia riziki yake ya kila siku.

Harmonize mwanzoni alibeba maji ili kupata tonge la chakula, pia alikuwa akiuza kahawa kwa wafanyabiashara wengine na wakazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam kabla ya sauti yake kutambulika mitaani. Kisha kuchukuliwa na lebo ya Diamond Platnumz ijulikanayo kama WCB. Kwa sasa ameamua kujiondoa katika lebo hiyo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Alianza kujihusisha na muziki mnamo mwaka 2011 ambapo alitoa nyimbo mbalimbali lakini hazikuweza kupata umaarufu mkubwa mpaka pale ambapo alikutana na Diamond Platinumz mnamo mwaka 2015 na kuanza kufanya muziki pamoja naye.

Harmonize ndiye mwanamuziki aliyetoa albamu yenye nyimbo 18 akiwa amewashirikisha Yemi Alade wa Nigeria na albamu hiyo inaitwa Afro East.

Mahusiano ya Harmonize

[hariri | hariri chanzo]

Harmonize alianza mahusiano na muigizaji maarufu wa Tanzania, Kajala Masanja, mwaka 2021.

Uhusiano wao ulivuma mitandaoni, huku Harmonize akimpa Kajala zawadi za kifahari, ikiwa ni pamoja na gari aina ya Range Rover. Hata hivyo, mahusiano yao yaliingia doa mwishoni mwa mwaka 2021 kutokana na madai ya usaliti. Harmonize alikiri hadharani kuwa alifanya makosa na kumwomba Kajala msamaha kwa njia tofauti, ikiwemo kuweka mabango makubwa ya kuomba msamaha jijini Dar es Salaam. Mwaka 2022, wawili hao walirudiana na hata kukubaliana kuchumbiana, lakini walitengana tena mwanzoni mwa 2023 kwa sababu zisizojulikana rasmi. Paula Kajala Kabla ya kurudiana na Kajala, Harmonize alihusishwa kimapenzi na Paula Kajala, ambaye ni binti wa Kajala Masanja, Tuhuma hizi zilisababisha mvutano mkubwa kati ya Kajala na Harmonize, huku Kajala akimshutumu Harmonize kwa kujaribu kumtongoza binti yake. Uhusiano wa Sasa Harmonize hajaweka wazi taarifa kuhusu uhusiano wake wa sasa. Amekuwa akijikita zaidi kwenye kazi yake ya muziki, huku akionekana kuepuka kufichua maisha yake ya mapenzi kwa umma.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
Nambari Mada ya wimbo Mwaka
1. Aiyola 2015[1]
2. Bado ft Diamond Platnumz 2016
3. Matatizo 2017
4. Happy Birthday 2017
5. Shula 2017
6. Sina 2017
7. Niambie 2017
8. Dont go 2017
9. Nishachoka 2017
10. Nakupenda 2017
11. Kwa ngwaru ft. Diamond platnumz 2018
12. Dm chick 2018
13. Atarudi 2018
14. Paranawe ft. Rayvanny 2018
15. Niteke 2019
16. Show me what you gat ft. Yemi Alade 2019
17. Kainama ft. Diamond Platnumz na Burna boy 2019
18. Ndoenda 2019
19. Never give up 2019

|20. |Mdomo |2021

Tuzo na teuzi

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Kazi iliyoteuliwa Tuzo Matokeo
2016 Bado Ft Diamond Platnumz WatsUp TV Tuzo la Video Bora zaidi ya Mwimbaji Chipukizi Ameshinda[2]
Yeye Mwenyewe African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) kwa Mwimbaji Chipukizi Ameshinda[3]
African Entertainment Awards (AEAUSA) kwa Msanii Chipukizi Bora zaidi Ameshinda[4]
  1. "Harmonize on Apple Music". iTunes (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2017-09-07.
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-24. Iliwekwa mnamo 2017-11-29.
  3. "Full List Of The AFRIMMA Awards 2016 Winners - HBR 103.5FM". 17 Oktoba 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-12. Iliwekwa mnamo 2017-11-29.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "African Entertainment Awards USA Full Nominees List". 2 Septemba 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-07. Iliwekwa mnamo 2017-11-29.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Harmonize kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.