Kabaka
Kabaka ni cheo cha mfalme wa Buganda ambayo ni ufalme ndani ya jamhuri ya Uganda. Cheo kingine pamoja na Kabaka ni Ssebataka.
Tangu mwisho wa karne ya 19 Makabaka wamekuwa Wakristo Waanglikana wakipokea taji katika kanisa kuu la Kianglikana la Kampala. Makabaka wa mwisho wamezikwa katika makaburi ya Kasubi mjini Kampala.
Serikali ya kwanza ya Milton Obote ilifuta falme zote nne za Uganda na kumlazimisha Kabaka Mutesa II kuondoka Uganda akipata kimbilio lake Uingereza.
Kati ya 1967 hadi 1993 cheo cha Kabaka hakikuwepo kisheria nchini Uganda lakini Waganda wengine walisikitikia. Serikali ya Yoweri Museveni ilirudisha falme za kale kama enzi za kiutamaduni.
Tarehe 24 Julai 1993 Ronald Muwenda Mutebi II aliruhusiwa kurudi Uganda kutoka Uingereza alikokuwa amemfuata baba yake akapokea rasmi taji la Kabaka mjini Kampala.
Makabaka wa Buganda
[hariri | hariri chanzo]- Kintu Kato, mwisho wa karne ya 14 BK
- Chwa I, mwanzo wa karne ya 15
- Kimera, takriban 1420 - takriban 1447
- Ttembo, takr. 1447 - takr. 1474
- Kiggala, takr. 1474 - takr. 1501
- Kiyimba, takr. 1501 - takr. 1501
- Kayima, takr. 1528 - takr. 1528
- Nakibinge, takr. 1555 - takr. 1582
- Mulondo, takr. 1582- mwisho wa karne ya 16
- Jjemba, mwisho wa karne ya 16
- Ssuuna I, mwanzo wa karne ya 17 - takr. 1609
- Ssekamanya, takr. 1609 - sehemu ya kwanza ya karne ya 17
- Kimbugwe, sehemu ya kwanza ya karne ya 17
- Kateregga, takr. 1636 - takr. 1663
- Mutebi I, Jjuuko, na Kayemba takr. 1663 - takr. 1690
- Tebandeke na Ndawula, takr. 1690 - takr. 1717
- Kagulu, Kikulwe na Mawanda. takr. 1717 - takr. 1744
- Mwanga, Namugala, na Kyabaggu, takr. 1744 - takr. 1771
- Jjunju na Ssemakokiro, takr. 1771 - 1797
- Ssemakokiro (pekee yake), takr. 1797 - 1814
- Kamanya, 1814 - 1836
- Suna II, 1836 - 1856
- Mutesa I, 1856 - 1884
- Mwanga II, 1884 - 1888
- Kiwewa Mutebi II, 1888 - alijiita kabaka bila kukubaliwa na wote wakati wa Mwanga II kukaa nje
- Kalema. 1888 - 1889 - alijiita kabaka bila kukubaliwa na wote wakati wa Mwanga II kukaa nje
- Mwanga II (mara ya pili) 1889 - 1897 – aliporudi kutoka nje baada ya kuuawa kwa Kiweewa Mutebi na Kalema na wafuasi wake
- Daudi Cwa II, 1897 - 1939
- Mutesa II, 1939 - 1969
- Miaka bila Kabaka 1969 - 1993
- Muwenda Mutebi II, 1993 – Kabaka aliyeko
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- en: Maelezo maupi juu ya Buganda kwa www.myuganda.co.ug Archived 14 Aprili 2004 at the Wayback Machine.
- en: Buganda.com
- en: Utamaduni wa Uganda