Nenda kwa yaliyomo

Kebo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kebo ya umeme
Kebo ya baharini ya mawasiliano

Kebo (kutoka Kiing. cable) ni muunganisho wa nyaya zilizofunikwa kwa mpira au plastiki ambazo hutumiwa kupitishia umeme, simu, au ishara za nuru[1].

Kazi ya kebo ni ama kubeba nishati au ishara za habari.

Nyaya za kupitisha umeme kwa kawaida ni za shaba, alumini au aloi za metali. Kebo za kupitisha data siku hizi hutumia hasa nyuzi za kioo zinazopitisha ishara za nuru.

Nyaya ndani ya kebo ni lazima kutengwa kwa vihami kati yake vinavyozuia kuingiliana kwa mikondo ya umeme au ishara za habari[2].

Kama kebo inayoathiriwa na nguvu za nje inahitaji kuimarishwa.

Marejeo

  1. What is a cable assembly?, tovuti ya aboutmechanics.com
  2. Definition coaxial cable, tovuti ya techtarget.com