Kim Jong-un
Kim Jong-un (matamshi ya Kikorea: [kim.dzʌŋ.ɯn] au [kim.tsʌŋ.ɯn]; alizaliwa 8 Januari 1982-1984 au 5 Julai 1984) ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea (WPK) na kiongozi mkuu wa Korea ya Kaskazini.
Kim ni mtoto wa pili wa Kim Jong-il (1941-2011) na Ko Yong-hui. Kabla ya kuchukua madaraka, Kim alikuwa haonekani mara kwa mara kwa umma. Maelezo kama vile mwaka gani alizaliwa, na kama alienda kweli shule nchini Uswisi akitumia jina la uongo, ni vigumu kuthibitisha.
Tangu mwaka 2009 taarifa zilianza kutokea kuwa Kim aliteuliwa kumfuata baba yake aliyekuwa mgonjwa, akipewa nafasi katika kamati ya kijeshi[1]. Nyimbo zilianza kutungwa za kusifu familia ya Kim zikitaja jina la Kim Jong-Un.[2] Mwaka 2010 alipewa cheo cha jenerali jeshini na kuwa makamu wa mwenyekiti wa kamati kuu ya kusimamia jeshi.
Kim alitangazwa kuwa kiongozi mkuu baada ya mazishi ya baba yake tarehe 28 Desemba 2011. Vyeo vyake ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea, Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi, Mwenyekiti wa Tume ya Mambo ya Ndani, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Watu wa Korea, na mwanachama wa Kamati ya Kudumu ya Politburo ya Chama cha Wafanyakazi wa Korea. Mnamo tarehe 9 Machi 2014, Kim Jong-un alichaguliwa bila kupingwa kuingia katika Bunge Kuu la Watu. Kim ana shahada mbili, moja ya fizikia kutoka Chuo Kikuu cha Kim Il-sung, na nyigine kama afisa wa Jeshi katika Chuo Kikuu cha Jeshi cha Kim Il-sung.
Tarehe 12 Desemba 2013, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vilitangaza kwamba kwa sababu ya "udanganyifu," aliamuru mauaji ya mjomba wake Jang Song-thaek. Kim Jong-un anaaminika kuwa ndiye aliyeamuru mauaji ya kaka yake wa kambo, Kim Jong-nam nchini Malaysia mwezi Februari 2017.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ In North Korea, Ailing Kim Begins Shifting Power to Military
- ↑ North Koreans sing praises of dynastic dictatorship
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Video kuhusu Kim Jon-un Archived 1 Desemba 2010 at the Wayback Machine.
- Muhtasari rasmi wa Kim Jong-un Archived 7 Novemba 2017 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kim Jong-un kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |