Kitenzi elekezi
Mandhari
Kitenzi elekezi ni kitenzi ambacho huchukua nomino ya mtendwa (yambwa). Yambwa ni jina au nomino ambayo huwakilisha mtendwa katika tungo.
Mfano: Mtoto anakula chakula. Katika tungo hiyo nomino chakula ni yambwa. Kitenzi anakula ni elekezi kwa kuwa kimeweza kuchukua mtendwa mbele yake.
Mfano wa pili: Juma anacheza muziki. Kitenzi anacheza ni elekezi kwa kuwa kimebeba mtendwa muziki.
Kwenye lugha ya Kiswahili, yambwa zipo za aina mbili:
- Yambwa tendwa, ni yambwa ambayo huonesha mtendwa ameathiriwa zaidi na jambo. Mfano: Mama anapika chakula. Nomino chakula ni yambwa tendwa kwa kuwa imeathirika. Sentensi hiyo unaweza kuigeuza na kusema, Chakula kimepikwa na mama. Hivyo, neno chakula limetendwa.
- Yambwa tendewa, ni yambwa ambayo huonesha nomino au jina ambalo limefaidika na jambo. Mfano: Baba alimpikia mama. Nomino mama imefaidika na tendo. Ndiyo maana tunasema yambwa tendewa.
Katika tungo yambwa hujulikana pia kama Shamirisho
Katika kamusi elekezi huwakilishwa na kifupisho ele.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitenzi elekezi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |