Mambo No. 5
“Mambo No. 5” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya Lou Bega kutoka katika albamu ya A Little Bit of Mambo | |||||
Imetolewa | 19 Aprili 1999 (Ujerumani) 17 Agosti 1999 (kimataifa) | ||||
Muundo | CD single | ||||
Aina | Pop/Jazz | ||||
Urefu | 5:14 (toleo refu) 3:39 (uhariri wa redio) | ||||
Studio | Lautstark / BMG / RCA Records | ||||
Mtunzi | Pérez Prado Lou Bega Zippy Davids | ||||
Mtayarishaji | Goar B Frank Lio Donald Fact | ||||
Mwenendo wa single za Lou Bega | |||||
|
'Mambo No. 5' ni jina la wimbo wa msanii wa Kijerumani Lou Bega. Wimbo unatokana na msanii Pérez Prado, ambaye awali alitengeneza ala tupu, lakini baadaye Lou Bega akaichukua ala zile na kutia maneno yake. Wimbo huu wa Bega, uliwika sana huko nchini Marekani, Uingereza, na Australia, ambamo mote ulifikia chati namba 1 mnamo 1999.
Nchini Australia, wimbo ulishikiria nafasi ya kwanza kwa takriban wiki nane, na kuufanya kuwa wimbo bora na wa mauzo bora wa mwaka. Pia kushika chati kibao katika nchi za Ulaya, ikiwemo nyumbani kwake Bega, Ujerumani, na kuifanya rekodi hii kukaa katika chati za Ufaransa kwa takriban wiki 20 (umekaa zaidi ya wimbo wowote ule kwa chati za US au UK), na wimbo ukashika nafasi ya 3 katika chati za Billboard Hot 100 nchini Marekani kunako tar. 2 Novemba 1999 (baada ya kuingia katika 40 Bora mnamo tar. 24 Agosti).