Nenda kwa yaliyomo

Moe Dalz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Abdallah Musa Makongoro (anajulikana kwa jina la kisanii Moe Dalz; amezaliwa mji wa Dodoma, 28 Juni 1999)[1] ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mwandaaji wa muziki na mwandishi wa vitabu kutoka nchini Tanzania. Anatambulika kwa uwezo wa kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza katika nyimbo zake, kitu ambacho kinawavutia watu wengi waishio nje ya nchi ya Tanzania, kwa sababu ya Kiingereza kuwa ni moja ya lugha kubwa na maarufu inayozungumzwa ulimwenguni kote. Pia ni mfanyabiashara mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa kampuni Tanfruits International.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Moe Dalz alizaliwa na Sylvia John, pia Musa Makongoro ambaye ni mwalimu na mfanyabiashara. Moe Dalz ni kifupi cha jina la baba yake Musa (ambalo kifupi chake ni Moe) na jina lake halisi Abdallah.

Alianza kutumbuiza na kuimba akiwa na umri mdogo kabisa, kuanzia shule ya msingi alipo soma mpaka sekondari. Alimaliza elimu ya msingi katika Shule ya msingi Kimanga, baadaye akajiunga na shule ya sekondari Kikuyu na kuchaguliwa katika shule ya Pugu sekondari kwa masomo ya kidato cha 5 na 6. Baada ya hapo alijiunga Dar es Salaam Institute of Technology, Dar es Salaam, Tanzania.

Maisha yake ya kimuziki yalianzia shule ya sekondari ambapo alianza kuimba covers za nyimbo maarufu kwa rafiki zake, na kuendelea kuimba kwa rafiki zake wa sekondari ambao walimsukuma kurekodi wimbo wake wa kwanza unaoitwa Hoi mwaka ,mnamo mwaka 2020.

Baadaye katika mwaka huo huo 2020 akiwa anasoma chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology,(DIT) na baada ya kujua haswa kipaji alichokuwa nacho alifanikiwa kurekodi wimbo mwingine ambao uliitwa "Closer" [2]. Wimbo huu ulitengenezwa na rafiki yake aitwaye Louis Richard Kombole (Luiz/Louis on the beat) na kufanyiwa mchanganyiko & uboreshaji na Cloud beats [3] ambaye ni mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania aliyefanya kazi chini ya kampuni ya kurekodi ya The industry label record chini ya Navykenzo. Wimbo Closer ni wimbo wake wa kwanza kuchezwa mara nyingi katika vituo vikubwa vya redio kama Clouds FM na Wasafi FM.

Januari 2022, Moe Dalz alitoa albamu yake ya kwanza (Albamu fupi(EP), ambayo inaitwa "Moe Dalz Unlocked" [4] [5], kwa sababu aliamini ule ulikuwa ndio muda sahihi wa kuachilia kipaji chake kwenye masikio ya wapenzi wa muziki. Hii ilimfungulia fursa kwa maana alianza kutambulika na watu wanaofanya kazi katika kiwanja cha burudani. Lakini kutokana na changamoto za hapa na pale alizozipata kama wasanii wengine wanavyozipata, aliamua kuanza kujifunza utayarishaji wa muziki, na kufanikiwa kuandaa, kuandika na kuimba wimbo unaoitwa "Allow Me".

Uandishi wa vitabu

[hariri | hariri chanzo]

Moe Dalz hakuishia katika muziki pekee, lakini pia mwaka 2022 aliandika vitabu viwili. Kitabu cha kwanza kuandikwa ni "Bring back my Theresa" [6] (Fiction) kikifuatiwa na "The art of being You" [7] (Educational book) ambacho kilikuwa na lengo la kusaidia vijana. Vitabu vyake vilimfanya aandikwe kwenye baadhi ya tovuti za Ghana [8] [9], ili kuelezea ni jinsi gani kijana anaweza akafanya kazi mbili kwa pamoja bila kuathiri mfumo wake wa maisha ya kila siku. Mwaka 2023 kitabu chake cha The Royal Tour with President Samia Suluhu Hassan kilitumika kufatilia safari ya Raisi Samia kwenye gazeti na tovuti ya daily nation kenya kutokana na mazungumzo aliyozungumza bungeni.

Kwa sasa Moe Dalz ameazimia kuandika vitabu zaidi kuhusu ujasiriamali, biashara na muziki, vitabu ambavyo vitasaidia zaidi hasa jamii za Afrika.

  • Moe Dalz Unlocked (2022)
  • Bring back my Theresa (2022)
  • The art of being You (2022)
  1. https://www.musicinafrica.net/directory/moe-dalz
  2. [1]
  3. [2]
  4. https://open.spotify.com/album/1wPjGUEjdqypnlBBnOtUS1?autoplay=true
  5. [3]
  6. [4]
  7. [5]
  8. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-03-31. Iliwekwa mnamo 2023-01-01.
  9. [6]