Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Moseskehengu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lugha
sw Mtumiaji huyu lugha mama yake ni Kiswahili.
en-2 This user is able to contribute with an intermediate level of English.


KWC Mtumiaji huyu ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
KWC Mtumiaji huyu ni mshiriki katika Shindano la Wikipedia ya Kiswahili la 2009.   (Submissions)


Jina langu kamili ni Moses Kehengu. Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ninayesomea shahada ya sayansi ya kompyuta. Nitamaliza elimu yangu mnamo mwezi wa tano mwaka 2010. Napendelea kusoma vitabu hasa vile vinavyozungumzia mada ambazo ni nje na masomo yangu. Kwa kusoma hivyo huwa inanisaidia kujua mambo mengine zaidi.

Madagascar:Escape 2 Africa :: Melman na Mfalme Julien

Pia mimi ni mpenzi mzuri wa kuangalia runinga hasa vipindi vya BBC. Napendelea makala ya Clickonline. Nafahamu mchezo wa tenisi ya meza kwa ustadi kiasi fulani. Mimi siyo bingwa sana wa mchezo wa huu, ila kama utakuwa hujafanya mazoezi siku nyingi, ukapocheza na mimi utaona ni mkali zaidi yako. Vilevile ni mpenzi wa sinema za vibonzo na zile za sayansi ya kufikirika.

Kwa ujuzi mimi ni mzoefu katika kuprogramu kompyuta kwa kutumia lugha mbalimbali za kompyuta kama vile C/C++, Java, PHP, HTML, CSS, Javascript, Visual Basic na C#. Pia na mengine mengi yanayohusiana na teknolojia ya mawasialiano na mtandao

Nimeaumua kushiriki katika shindano hili la kuandika makala za Kiswahili kwa sababu mimi mpenzi wa lugha yangu ya Kiswahili na nina mengi ya kutoa kwa jamii hasa yale ambayo naamini ni mageni ya kufurahisha. Naamini kwa kuendeleza kupitia shindano hili na baada ya shindano tutaweza kuongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya makala za kiswahili na kuongeza watumiaji wa lugha yetu ya thamani ya kiswahili katika mtandao.