Nenda kwa yaliyomo

Robert Fisk

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Robert Fisk (12 Julai 194630 Oktoba 2020) alikuwa mwandishi na mwanahabari raia wa Uingereza na Eire. Aliandika hasa kuhusu hali ya nchi za Mashariki ya Kati kuanzia mwaka 1976 hadi kifo chake.

Kuanzia 1989 hadi kifo chake, alikuwa mwandishi wa Independent. [1] Fisk alizaliwa Maidstone, Kent .

Fisk alisoma katika Chuo Kikuu cha Lancaster na katika Chuo cha Trinity Dublin.

Alijua vizuri sana lugha ya Kiarabu[2]. Alikuwa mmoja wa wanahabari wachache waliopata nafasi ya kumhoji Osama bin Laden. Alimhoji mara tatu kati ya miaka 1993 na 1997. [3]

Fisk alifariki kwa kiharusi mnamo 30 Oktoba 2020 katika hospitali ya Dublin, Ireland akiwa na umri wa miaka 74. [4]

  1. "Robert Fisk". The Independent (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-06-04.
  2. "Robert Fisk lecture (audio)". Fass.kingston.ac.uk. Faculty of Arts and Social Sciences – Kingston University London. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Mei 2013. Iliwekwa mnamo 21 Agosti 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Fisk, Robert. The Great War for Civilisation: The Conquest of the Middle East. Fourth Estate. ku. 1–39. ISBN 1-84115-007-X.
  4. "Veteran journalist and author Robert Fisk dies aged 74". 
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Robert Fisk kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.