Sifuri halisi
Sifuri halisi katika fizikia ni kiwango cha halijoto ya duni kabisa inayowezekana.
Ni sawa na vizio −273.15° kwenye skeli ya selsiasi au vizio 0° kwenye skeli ya kelvini.
Kwenye kiwango cha sifuri halisi hakuna mwendo wa maada au molekuli tena. Sababu yake ni ya kwamba halijoto yenyewe kifizikia ni uso mwingine wa mwendo wa mada yaani mwendo wa molekuli na atomi.
Katika hali ya kawaida molekuli za hewa au za kiowevu huwa na mwendo; pia molekuli za gimba mango huwa na mwendo fulani kama kitikisiko. Kama mwendo = halijoto inaongezeka tunaona badiliko la gimba mango kuwa kiowevu au gesi. Kinyume chake tunaona jinsi gani maji "baridi" huwa barafu imara maana yake mwendo wa molekuli za H20 imepungua. Pasipo mwendo tena hakuna joto wala halijoto na hali hii huitwa "sifuri halisi".
Hali hii inasababisha kutokea kwa mambo yasiyo kawaida. Kwa mfano uwezo wa metali wa kupitisha umeme unaongezeka sana kadiri metali inavyokaribia sifuri halisi.
Hali halisi haiwezekani kukuta mada kwenye hali ya sifuri halisi kabisa lakini katika maabara imewezekana kuikaribia sana.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sifuri halisi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |