Tatyana Ali
Tatyana Ali | |
---|---|
Tatyana Ali at the U.S. Presidential Inauguration (2009).
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Tatyana Marisol Ali[1] |
Amezaliwa | 24 Januari 1979 |
Asili yake | North Bellmore, Long Island, New York, Marekani |
Aina ya muziki | R&B, Soul, Dansi-Pop |
Kazi yake | Filamu, Mwigizaji wa televisheni Mwimbaji |
Miaka ya kazi | 1985 — hadi leo (mwigizaji) 1997 — hadi leo (mwibaji) |
Studio | MJJ/Work/SME Records (1997—2001) |
Ame/Wameshirikiana na | Will Smith |
Tovuti | tatyanaalionline.com |
Tatyana Marisol Ali (alizaliwa mnamo 24 Januari 1979) ni mwigizaji wa filamu na mwimbaji wa muziki wa R&B kutoka nchini Marekani. Huenda akawa anafahamika zaidi kwa kucheza kama Ashley Banks kutoka katika ucheshi wa Fresh Prince of Bel-Air, aliokuwa anaigiza na Will Smith.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Ali alizaliwa mjini Long Island, New York, Marekani, ni binti wa Sonia, mwuguzi, na Sheriff Ali, askari mpelelezi. Mama yake ni mzaliwa wa Panama na baba yake ni mhindi asilia kutoka Trinidad na Tobago. Ali pia ana wadogo zake wa kike wawili, mmoja anaitwa Anastasia mwingine anaitwa Kimberly. Ali ni mwongeaji mzuri wa Kiingereza na Kihispania.
Tatyana alipata elimu yake ya sekondari katika shule ya Marymount High School iliyopo magharibi mwa Los Angeles, California, na Buckley School iliyopo Sherman Oaks, Los Angeles, California. Mnamo mwaka wa 2002, Ali alihitimu Chuo Kikuu cha Harvard (Harvard University) na kupata digrii ya sayansi ya jamii.
Filamu alizoigiza Ali
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Filamu | Aliigiza kama | Maelezo |
---|---|---|---|
1987 | Eddie Murphy Raw | Dada yake Eddie | Kipande kifupi |
1988 | Crocodile Dundee II | Park Girl | |
1988 | Wow, You're a Cartoonist! | Child Cartoonist | Filamu fupi |
1997 | Fakin' da Funk | Karyn | |
1997 | Kiss the Girls | Janell Cross | |
1998 | The Clown at Midnight | Monica | |
1999 | Jawbreaker | Brenda | |
2000 | Brother | Latifa | |
2001 | The Brothers | Cherie Smith | |
2003 | National Lampoon Presents Dorm Daze | Claire | |
2004 | Nora's Hair Salon | Lilleana | |
2005 | Back in the Day | Alicia Packer | |
2005 | Domino One | Laeticia Richards | |
2006 | Glory Road | Tina Malichi | |
2006 | A Warm Place | Clair Andrews | Filamu fupi |
2007 | The List | Cynthia | |
2008 | Down & Out | Filamu fupi | |
2008 | Nora's Hair Salon 2: A Cut Above | Lilleana | |
2008 | Hotel California | Jessie | |
2009 | Mother and Child | Maria | |
2010 | Pete Smalls Is Dead | Cocktail Waitress | |
2012 | Privileged | Talia | |
2012 | Dysfunctional Friends | Alex | |
2012 | Home Again | Marva Johnson | |
2013 | 24 Hour Love | Simply | |
2013 | The Last Letter | Jillian | |
2014 | Locker 13 | Lucy | |
2015 | November Rule | Leah |
Almbamu alizotoa
[hariri | hariri chanzo]- Kiss the Sky (1998)
- The Light (2007)
Nyimbo maarufu
[hariri | hariri chanzo]- "Daydreamin'" - #5 US, #6 UK
- "Boy You Knock Me Out" (Akishirikiana na Will Smith) - #3 UK
- "Everytime" - #20 UK
- "It's All Right"/"Somebody Loves You" - Bado kutolewa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Tatyana Ali at NNDB". NNDB.com. Iliwekwa mnamo 2007-09-24.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu muziki wa Marekani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tatyana Ali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |