Vitamini A
Mandhari
Vitamini A ni aina ya vitamini ambayo hupatikana kwenye baadhi ya matunda na mizizi kwa ajili ya kusaidia uwezo wa macho kuona.
Mfano wa mzizi wenye vitamini A ni karoti; mfano wa mboga ni mchicha; mfano wa matunda tajiri katika vitamini A ni chungwa n.k.
Yapo madhara yanayotokana ukosefu au upungufu wa vitamini A; miongoni mwa madhara hayo ni magonjwa kama vile "ukavu macho".
Madhara ya ugonjwa huo ni kama vile:
- 1. macho kuwasha
- 2. macho kushindwa kuona ipasavyo hasa usiku.
- 3. kukauka kwa ngozi.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vitamini A kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |