Wentworth Miller
Wentworth Miller | |
---|---|
Wentworth mnamo Septemba 2011 | |
Amezaliwa | 2 Juni 1972 Chipping Norton, Oxfordshire, Uingereza |
Miaka ya kazi | 1998–hadi leo |
Wentworth Earl Miller III (amezaliwa tar. 2 Juni 1972) ni mwigizaji wa filamu wa Kimarekani-Kiingereza, aliyetunukiwa tuzo ya Golden Globe akiwa kama mwigizaji bora wa filamu na tamthiliya. Amejizolea umaarufu mkubwa baada ya kucheza kama Michael Scofield kutoka katika tamthilia ya Prison Break iliyokuwa inarushwa hewani na televisheni ya FOX Network.
Maisha yake na wasifu
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Miller alizaliwa Chipping Norton, Oxfordshire, Uingereza, ambapo baba yake alikuwa akiishi huku akisoma katika chuo cha Oxford. Familia yake baadae ilihamia Park Slope, Brooklyn, New York, kipindi ana mwaka mmoja. Ana madada wawili, Leigh na Gillian. Alipata elimu yake pale Midwood High School iliyopo Brooklyn, New York USA. Alihitimu masomo yake katika Chuo cha Princeton akiwa na shahada ya Fasihi ya Kiingereza.
Katika mahojiano, Miller alibainisha kuwa asili yake ni mchanganyiko. Akimaanisha kuwa baba yake ni Mmarekani-Mwafrika, Muingereza, Muitalia, Mjerumani na nusu Mcherokee[1] na mama yake ni Mrusi, Mfaransa, Mdachi na Msyria.
Maisha ya Uigizaji
[hariri | hariri chanzo]Miller kwa mara ya kwanza aliigiza nafasi ya nyota kama David katika tamthilia fupi Dinotopia ya ABC. Baada ya kuonekana katika maigizo tofauti tofauti ya kwenye runinga, alihamia kwenye filamu ya mwaka 2003 The Human Stain akicheza nafasi ya nyota msaidizi. Aliigiza kama Anthony Hopkins kijana. Miller alianza kuonekana kwenye runinga kwenye tamthilia ya Buffy the Vampire Slayer (Go Fish 1998).
Mwaka 2005, Miller alicheza kama Michael Scofield kwenye tamthilia ya Prison Break ya FOX Network. Amigiza kama kaka anayemjali nduguye kwa kuandaa na kufanikisha mpango mzima wa kumtorosha jela kaka yake Lincoln Burrows ili kumuepusha na adhabu ya kifo aliyohukumiwa kimakosa. Umahiri aliouonyesha kwenye tamthilia hiyo ulipelekea kujipatia tuzo ya Golden Globe 2005 kwa kuchaguliwa kuwa Muigizaji Bora wa Kiume Kwenye Tamthilia.[2] Miller ameonekana kwenye video mbili za muziki za mwanadada Mariah Carey na alipata mchango mkubwa kutoka kwa Carey kutokana na video ya nyimbo We Belong Together. Miller anadai kuwa umahiri wa video hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa kuwashawishi waandaaji kumpa nafasi ya nyota kwenye tamthilia iliyojizolea umaarufu ya Prison Break. Anasema, "Mariah ni maarufu kimataifa. Siku mbili nilizokuwa naigiza kwenye video zake zimenisaidia sana kisanaa, zimenitangaza zaidi kuliko jambo lolote nililowahi kulifanaya kabla ya Prison Break. Ninashukuru sana kwa nafasi ile."
Filamu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina | Kama | Maelezo |
---|---|---|---|
Tamthilia | |||
1998 | Buffy the Vampire Slayer | Gage Petronzi |
|
2000 | ER | Mike Palmieri |
|
2000 | Time of Your Life | Nelson |
|
2002 | Dinotopia | David Scott | Tamthilia fupi |
2005 | Ghost Whisperer | Sgt. Paul Adams |
|
2005 | Joan of Arcadia | Ryan Hunter |
|
2005–Sasa | Prison Break | Michael Scofield | Tamthilia |
Filamu | |||
2001 | Room 302 | Server #1 | Filamu fupi |
2003 | Underworld | Dr. Adam Lockwood | |
2003 | The Human Stain | Coleman Silk mdogo | |
2005 | Stealth | voice of EDI | |
2005 | The Confessions | Prisoner | Short film |
Video za Miziki | |||
2005 | "It's like That" | Mysterious love interest | Video ya Muziki ya Mariah Carey |
2005 | "We Belong Together" | Mysterious love interest | Video ya Muziki ya Mariah Carey |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Christopher Loudon, "Wentworth Miller's Big Break", Sir. Canada's International Magazine of Style for Him, Spring 2006, p. 61.
- ↑ "2006 Golden Globe Nominations & Winners". Hollywood Foreign Press Association. Januari 26 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-02-17. Iliwekwa mnamo 2007 02 26.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
na|date=
(help)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Wentworth Miller at the Internet Movie Database
- Wentworth Miller katika Movies.com
- Wentworth Miller's biography Archived 14 Aprili 2009 at the Wayback Machine. at Prison Break's official website
- Interview with Wentworth on WHO.com Archived 27 Septemba 2007 at the Wayback Machine.