Nenda kwa yaliyomo

Yericko Y. Nyerere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yericko Nyerere

Amezaliwa 14 Aprili 1983
Iringa, Tanzania
Nchi Tanzania
Kazi yake Muandishi wa vitabu
Chama cha kisiasa CHADEMA

Yericko Yohanesy Msambila Mkana Nyerere (alizaliwa katika Kijiji cha Maduma, wilaya ya Mufindi, mkoa wa Iringa, Tanzania, 4 Aprili 1983), ni mfanyabiashara mwanzilishi wa kampuni ya "Yecco Group Limited". Ni mwanachama na mjumbe wa Mkutano Mkuu wa chama cha kisiasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Yericko Yohanesy Nyerere ni mshindi wa tuzo 5 mfululizo "Barani Afrika", ambapo tuzo 4 ni za "Mwandishi Bora wa Vitabu Afrika", na tuzo 1 ni ya "Kiongozi Bora wa Kijamii Afrika", tuzo za "Zikomo Africa Awards" 2023 na 2024 alishinda mara tatu, tuzo ya "Shining Stars Africa Awards" 2024 alishinda mara moja, na tuzo ya "Music Video Africa Awards" (MVAA) akishinda mara moja.

Tuzo za uandishi wa vitabu alishinda kupitia kitabu chake cha "Ujasusi wa Kidola na Kichumi", toleo la 2016 na kitabu cha "Moscow Operesheni Ukraine" toleo la 2024 pia ameandika vitabu kama "Mapambano ya Madaraka", toleo la 2017, "Strategy The Road to Power", toleo la 2018, na kitabu cha "Mtu Baada ya Mtu", toleo la 2020. [1] Yericko pia amejinasibu hadharani kuwa anaabudu dini za Kiafrika za asili (Mizimu). Hivyo yeye si "Mkristo" wala "Muislamu".

Urithi wake wa fasihi juu ya uandishi pia unadhihirishwa juu ya mkakati wa ushindi wa ushirika wa vyama wa vyama pinzani nchini Tanzania (UKAWA) wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015 akiwa sehemu ya jopo la wanamikakati wa Chama.

Yericko ana Stashahada ya Saikolojia ya kiuchunguzi kutoka katika chuo kikuu huria cha Uingereza (2016-2017), akapata Stashahada ya Uchunguzi na Upelelezi kutoka taasisi ya kimataifa ya Uchunguzi na upelelezi ya "International Institute Of Certified Forensic Investigation Professionals" kwa kushirikiana na "Osulivan Associates International" - USA (2015).

Tangu 2010 hadi Julai 2015, Yericko Nyerere alikuwa mshauri wa Usalama na Ulinzi binafsi kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Willibrod Peter Slaa. Kama mwanaharakati wa kisiasa anasifika kwa mazungumzo yake ya busara juu ya mabadiliko ya kisiasa na maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania, kazi zake hasa vitabu na makala mitandaoni zimesababisha ushawishi mkubwa kwa kura nyingi kwa watoa maamuzi na viongozi wa kisiasa. Amekuwa msukumo wa kisiasa kwa mabadiliko na ushiriki wa vijana na ushiriki katika ajenda ya serikali na mabadiliko ya kiuchumi.

  1. "UU Ventures". www.uu.com. Iliwekwa mnamo 2024-12-18.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yericko Y. Nyerere kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.