Yoga
Yoga ni mazoezi ya kiroho na kimwili yenye asili katika falsafa ya Uhindi. Tangu miaka ya 1980 yoga ilisambaa pia nje ya Uhindi katika nchi za magharibi kama mazoezi ya kimwili. Katika utamaduni wa Kihindi yoga inatekelezwa pamoja na jitihada za kiroho na kidini kwenye msingi wa Uhindu na pia Ubuddha. Mtu anayefanya mazoezi ya yoga huitwa yogi.
Shabaha za Yoga
[hariri | hariri chanzo]Shabaha ya mazoezi ya yoga ni kujikamilisha kama binadamu mwenye mwili, nafsi na roho. Hapa ni wazo muhimu kutawala tamaa za mwili na roho zinazotazamiwa kama kizuizi kwenye njia ya kufikia ukamilifu. Kwa hiyo mwanafunzi wa yoga apate kujifunza nidhamu ya ndani na nidhamu ya kimwili.
Njia muhimu kuelekea shabaha hii ni kufanya mazoezi ya kudhibiti pumzi na kumakinisha fikra na hisia. Watendaji na walimu wa yoga huamini ya kwamba mazoezi haya yanachangia kwenye afya ya kimwili na kiroho. Kujifunza mikao fulani ya mwili ni mbinu ya kufikia shabaha za yoga.
Yoga katika Magharibi
[hariri | hariri chanzo]Yoga ilisambazwa na walimu kutoka Uhindini katika Ulaya na Marekani. Katika nchi hizi za magharibi ni zaidi mazoezi ya kimwili na elimu ya mikao yaliyopokelewa bila kuelewa asili katika roho ya Uhindu na falsafa yake. Yoga imependekezwa kama mbinu za kunpunza matatizo ya afya, kuimarisha musuli na hasa uti wa mgongo kwa watu wanaoketi muda mrefu ofisini, na kupunguza dhiki na shinikizo ya maisha ya kisasa (stress). Kwa hiyo matumizi yayoga inafanana kiasi na aina ya michezo.
Yoga na dini nyingine
[hariri | hariri chanzo]Kiasi mazoezi ya yoga yanaweza kufanana na taamuli za kiroho jinsi zinavyopatikana pia katika dini kama Ukristo na Uislamu.
Ubuddha
[hariri | hariri chanzo]Madhehebu kadhaa za Ubuddha yanajua mazoezi yanayofanana na yoga, hasa upande wa Zen. Hapa njia za kutawala pumzi na fikra zinafundishwa pia, pamoja na mikao mbalimbali ya mwili. Ilhali kulikuwa na kipindi ca athira kubwa ya Kibuddha katika Uhindi inawezekana ya kwamba sehemu za mazoezi ya Yoga zina asili katika Ubuddha.
Ukristo
[hariri | hariri chanzo]- Kuna wakristo wanaotoa onyo dhidi ya matumizi ya yoga wakikazia asili yake katika Uhindu[1]
- katika kanisa katoliki mazoezi ya yoga yametumiwa kwa idhini ya papa na maaskofu ndani ya mazoezi ya kiroho[2]
Uislamu
[hariri | hariri chanzo]- walimu na viongozi mbalimbali wa Uislamu wamekataza matumizi ya yoga, kwa mfano Misri, Indonesia na Malaysia[3]
- jumuiya za Wasufi wanatumia mbinu za kusimamia pumzi na mikao kadhaa yenye asili katika yoga. [4]
Mifano ya mazoezi ya yoga
[hariri | hariri chanzo]-
Sanamu ya mungu Siva katika mkao wa Yoga
-
Mazoezi ya kwanza ya yoga katika kikundu cha wanafunzi huko Marekani
-
Mkao mgumu wa yoga kwa watu wawili
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Dr Ankerberg, John & Dr Weldon, John, Encyclopedia of New Age Beliefs, Harvest House Publishers, 1996
- ↑ Trying to reconcile the ways of the Vatican and of te East, New York Times January 7, 1990
- ↑ "Fatwa ya Halmashauri Kuu ya Waislamu wa Malaysia inatangaza yoga kuwa haraam, ikitofautisha na mazoezi ya kimwili tu". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-22. Iliwekwa mnamo 2008-12-22.
- ↑ "Carl W. Ernst, Situating Sufism and Yoga, review of article in Journal of the Royal Asiatic Society, Third Series, Vol. 15, No. 1 (Apr., 2005), pp. 15- 43" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-08-24. Iliwekwa mnamo 2015-05-21.
Kujisomea
[hariri | hariri chanzo]- Bryant, Edwin (2009). The Yoga Sutras of Patañjali: A New Edition, Translation, and Commentary. New York, USA: North Point Press. ISBN 978-0865477360.
- Crangle, Edward Fitzpatrick (1994), The Origin and Development of Early Indian Contemplative Practices, Otto Harrassowitz Verlag
- Dhillon, Dalbir Singh (1988). Sikhism, Origin and Development. Atlantic Publishers. GGKEY:BYKZE4QTGJH.
- De Michelis, Elizabeth (2004). A History of Modern Yoga. London: Continuum. ISBN 0-8264-8772-6.
- Dumoulin, Heinrich; Heisig, James W.; Knitter, Paul F. (2005). Zen Buddhism: a History: India and China. World Wisdom, Inc. ISBN 978-0-941532-89-1.
- Eliade, Mircea (1958). Yoga: Immortality and Freedom. Princeton: Princeton University Press. ISBN 978-0-691-14203-6.
- Feuerstein, Georg (1996). The Shambhala Guide to Yoga. 1st ed. Boston & London: Shambhala Publications.
- Flood, Gavin D. (1996), An Introduction to Hinduism, Cambridge University Press
- Goldberg, Philip (2010). American Veda. From Emerson and the Beatles to Yoga and Meditation. How Indian Spirituality Changed the West. New York: Harmony Books. ISBN 978-0-385-52134-5.
- Flood, Gavin (1996). An Introduction to Hinduism. Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 0-521-43878-0.
- Gambhirananda, Swami (1998). Madhusudana Sarasvati Bhagavad_Gita: With the annotation Gūḍhārtha Dīpikā. Calcutta: Advaita Ashrama Publication Department. ISBN 81-7505-194-9.
- Jacobsen, Knut A.; Larson, Gerald James (2005). Theory And Practice of Yoga: Essays in Honour of Gerald James Larson. BRILL. ISBN 978-90-04-14757-7.
- Larson, Gerald James (2008). The Encyclopedia of Indian Philosophies: Yoga: India's philosophy of meditation. Motilal Banarsidass. ISBN 978-81-208-3349-4.
- Lidell, Lucy (1983). The Sivananda Companion to Yoga (PDF). London: Gaia Books Limited. ISBN 0-684-87000-2.
- McEvilley, Thomas (2002). The shape of ancient thought. Allworth Communications. ISBN 978-1-58115-203-6.
- Müller, Max (1899). Six Systems of Indian Philosophy; Samkhya and Yoga, Naya and Vaiseshika. Calcutta: Susil Gupta (India) Ltd. ISBN 0-7661-4296-5. Reprint edition; Originally published under the title of "The Six Systems of Indian Philosophy."
- Possehl, Gregory (2003). The Indus Civilization: A Contemporary Perspective. AltaMira Press. ISBN 978-0-7591-0172-2.
- Radhakrishnan, S.; Moore, CA (1967). A Sourcebook in Indian Philosophy. Princeton. ISBN 0-691-01958-4.
- Samuel, Geoffrey (2008), The Origins of Yoga and Tantra, Cambridge University Press, ISBN 978-0-521-69534-3
- Satyananda, Swami (2008). Asana Pranayama Mudra Bandha (PDF). Munger: Yoga Publications Trust. ISBN 978-81-86336-14-4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-08-07. Iliwekwa mnamo 2015-05-21.
{{cite book}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Taimni, I. K. (1961). The Science of Yoga. Adyar, India: The Theosophical Publishing House. ISBN 81-7059-212-7.
- Werner, Karel (1998). Yoga And Indian Philosophy (1977, Reprinted in 1998). Motilal Banarsidass Publ. ISBN 81-208-1609-9.
- Whicher, Ian (1998). The Integrity of the Yoga Darśana: A Reconsideration of Classical Yoga. SUNY Press. ISBN 978-0-7914-3815-2.
- White, David Gordon (2011), Yoga, Brief History of an Idea (Chapter 1 of "Yoga in practice") (PDF), Princeton University Press
- Worthington, Vivian (1982). A History of Yoga. Routledge. ISBN 0-7100-9258-X.
- Wynne, Alexander "The Origin of Buddhist Meditation." Routledge, 2007, ISBN 1-134-09741-7.
- Zimmer, Heinrich (1951), Philosophies of India, New York, New York: Princeton University Press, ISBN 0-691-01758-1 Bollingen Series XXVI; Edited by Joseph Cambell.
- Zydenbos, Robert. Jainism Today and Its Future. München: Manya Verlag, 2006. p. 66
- Tovuti ya mwalimu wa yoga Kriya Yoga Mahavatar Babaji