Nenda kwa yaliyomo

Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki

Majiranukta: 2°46′43″S 38°46′18″E / 2.77861°S 38.77167°E / -2.77861; 38.77167
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki
Mahali pa Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki
MahaliKenya
Coordinates

2°46′43″S 38°46′18″E / 2.77861°S 38.77167°E / -2.77861; 38.77167{{#coordinates:}}: cannot have more than one primary tag per page

Eneo11,747 km²
Kuanzishwa1948
Mamlaka ya utawalaKenya Wildlife Service
Tembo kuvuka barabara katika Tsavo Mashariki
Mlango wa kuingia Mbuga ya Kitaifa ya Bachuma Tsavo

Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki ni moja ya hifadhi kubwa zaidi na kongwe nchini Kenya iliyotambaa eneo la kilomita za mraba 11,747. Ilifunguliwa mnamo Aprili 1948, na iko karibu na kijiji cha Voi katika Kaunti ya Taita-Taveta. Hifadhi hii imegawanywa katika sehemu za mashariki na magharibi na barabara na reli ya A109. Jina lake ambalo linatokana mto Tsavo, ambao unatiririka kutoka magharibi hadi mashariki kupitia hifadhi hii, iko mpakani mwa Hifadhi ya Taifa ya milima ya Chyulu, na hifadhi ya wanyama ya Mkomazi nchini Tanzania.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Mguga hii yaweza kuingiwa kupitia milango kuu tatu, kutoka Voi kupitia mlango wa Manyani, kutoka Mombasa kupitia mlango wa Bachuma au kutoka Malindi kupitia mlango wa Sala. Pia kuna nyanja kadhaa za ndege katika mbuga hii zinazo ruhusu ndege ndogo kutua. Ndani ya mbuga, mito Athi na Tsavo huungana na kuunda Mto Galana. Sehemu kubwa ya mbuga inajumuisha jangwa na savanna. Mbuga hii inaaminika kuwa ni moja ya hifadhi kubwa yenye viumbe mbalimbali na tofauti hai duniani, na umaarufu wake zaidi hutokana na kiasi kikubwa cha wanyamapori mbalimbali wanaopatikana katika mbuga hii. Mbuga hii pia ina pointi au sehemu kadhaa ambapo watu waweza kupiga kambi na pointi kadhaa za kijiografia zenya riba.

Sehemu kubwa ya Tsavo Mashariki kwa ujumla ni tambarare kavu ambapo mto Galana hutiririka. Baadhi ya vitu vingine muhimu kataka mbuga hii ni Bie ya Yatta na mtiririko wa maji wa Lugards. Baadhi ya wanyamapori katika mbuga hii ya Tsavo Mashariki ni kama vile vifaru weusi na kongoni aina ya hirola.

Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Magharibi ina milima zaidi na mabwawa kuliko ile ya mashariki na pia ina chemchemi za maji za Mzima na Ziwa la Jipe. Inajulikana sana kwa kuwa na ndege wengi na kwa mamalia wakubwa. Pia ni nyumbani kwa vifaru weusi.

Akiolojia / Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ingawa maeneo chache ya akiolojia ya awali ya Stone Age na Middle Stone Age zimerekodiwa kutoka kwa ardhi inayopatikana katika sehemu ya Tsavo, kuna ushahidi wa kutosha kuonyesha uchumi unapendelea wa Late Stone Age kutoka miaka 6,000 hadi 1,300 iliyopita. Utafiti umeonyesha kwamba maeneo ya akiolojia ya Late Stone Age zinapatikana karibu na Mto Galana kwa wingi. Wenyeji wa maeneo haya waliwindwa wanyamapori, walivua samaki na pia kufunga wanyama wa kinyumbani. Kwa sababu ya upungufu wa maji kutoka Mto Galana, makazi ya binadamu katika Tsavo yalilenga sana maeneo yanayomiliki bonde hilo na katika eneo wazi ya mawe ukielekea magharibi.

Wafanyabiashara waswahili walifanya biashara na wenyeji wa Tsavo kwa kuuza na kununua pembe za ndovu, ngozi za wanyamapori na pengine watumwa mnamo miaka 700 Baada ya Kifo cha Kristo (na pengine mapema). Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba waswahili walikuwa wakoloni wa Tsavo. Badala yake, biashara iliimarishwa kupitia kupelekwa kwa bidhaa kutoka swahili ya pwani na pia kuondolewa kwa bidha kutoka Swahili ya pwani kupitia kupanuliwa kwa jamii. Biashara ya bidhaa kama vile gamba za kaa na mbanyoa zimekuwa zikipatikana kutoka maeneo ya akiolojia yaliyoanza mapema wakati wa kipindi hicho cha uswahili.

Karne ya kumi na tisa wapelelezi wa Kiingereza na hata wa Kijerumani waliandika kwamba watu ambao sasa tunawaita Orma na Waata wakati wa safari zao kupitia "nyika,", kwa ujumla wao walikuwa wanaonekana kama maadui kutokana na hisia zao. Kuanzia mwisho wa karne ya kumi na tisa / mapema karne ya ishirini, Waingereza walianza juhudi za kuwa wakoloni katika sehemu za ndani za Kenya na wakajenga reli ya Uganda kupitia Tsavo katika mwaka wa 1898. Ujenzi ulikwama kwa muda katika eneo la Tsavo mashariki wakati wa kujenga daraja juu ya mto Tsavo kwa sababu "simba walao wandamu" waliwashambulia wajenzi wa reli na simba hao walijulikana baada kama wala watu wa Tsavo.

Tsavo ilibakia ya nchi kwa wafugaji wa Orma na Wamasai na wawindaji na wakusanyaji wa Waata hadi mwaka wa 1948, wakati ilikubaliwa rasmi kama Mbuga ya Kitaifa. Wakati huo, idadi ya wazawa ilihamishwa kwa maeneo ya Mtito Andei na Voi na vilevile maeneo mengine karibu na Vilima vya Taita. Kufuatia uhuru wa Kenya mwaka wa 1963, uwindaji ulipigwa marufuku katika mbuga hii na usimamizi wa Tsavo ulisalimishwa kwa mamlaka ambayo hatimaye ikawa Kenya Wildlife Service. Tsavo sasa huvutia watalii wanaopiga picha kutoka kote duniani wenye riba ya kushauku upana wa jangwani na Mandhari ya ajabu.

Vivutio Kuu

[hariri | hariri chanzo]

Mwamba wa Mudanda

[hariri | hariri chanzo]

Mwamba wa Mudanda ni mwamba wa kilomita 1.6 na hutumika kama vyanzo vya maji vinavyosambaza bwawa wa asili chini. Mwamba huu huwa ni sehemu nzuri ya kuwatazama tembo ambao idadi yao nli takriban mamia kadhaa na wanyama wengine wa pori ambao huja kunywa maji wakati wa kiangazi.

Tambarare ya Yatta

[hariri | hariri chanzo]

Tambarare ya Yatta, mtiririko mrefu ulimwenguni wa lava, inapitia kando ya mpaka wa magharibi wa Mbuga juu ya Mto Athi. Urefu wake wa kilomita 290 uliundwa na lava kutoka Mlima wa Ol Doinyo Sabuk.

Mtiririko wa maji wa Lugard

[hariri | hariri chanzo]

Lugard Falls, ambalo lilipata jina lake baada ya Frederick Lugard, ni mfululizo wa mitiririko ya maji kwenye Mto Galana.

Bwawa la Aruba

[hariri | hariri chanzo]

Bwawa la Aruba lilijengwa mwaka wa 1952 katika Mto Voi. Hifadhi ya maji iliyoumbwa na bwawa huvutia wanyama wengi na ndege wengi wa maji.

Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo Mashariki ni mojawapo wa hifadhi za wanyama kubwa zaidi duniani, kwani hutoa makazi ya jangwani ambayo hayajaendelea kwa idadi kubwa ya wanyama. Orodha pana ya aina za wanyama ambao hupatikana katika Mguga hii ya Tsavo Mashariki inajumuisha fisi mdogo, nyani mashariki, popo, mbogo, komba, pongo, simbamangu, kimburu, duma, ngawa, digidigi, mbwa-mwitu wa Afrika, panya-miti, chesi, nsya, funo, pofu, tembo wa Afrika, mbweha, komba mkubwa, kinokera au swala, kanu madoa-makubwa kusi, kanu madoa-madogo, swala twiga, twiga, sungura wa Afrika, kamendegere, kongoni, hirola, kalunguyeye tumbo-jeupe, fisi madoa, fisi milia, perere kusi, pimbi mkubwa, swala pala, mbweha mweusi, mbweha milia, ngurunguru, tandala mdogo, chui, simba, nguchiro miraba, nguchiro mdogo, karasa, nguchiro-bwawa, nguchiro mkia-mweupe, tumbili, fisi-maji, kakakuona, nyegere, nungu wa Afrika, ndezi, buku, kifaru mweusi, kidiri, suni, gwasi, ndogoro na punda milia.

Kuna zaidi ya spishi 500 za ndege ambazo zimerekodiwa kutoka katika eneo hilo na ni pamoja mbuni , kozi , shakivale, kwenzi, kwera, kurea , fimbi, karani tamba na koikoi.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]