Mbuzi-kaya
Mbuzi-kaya | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mbuzi na mwanawe
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
|
Mbuzi-kaya ni mnyama katika ngeli ya mamalia ambaye huzaa na kunyonyesha mwenye miguu minne na mwenye tabia zinazofanana na ng'ombe. Kwa ukubwa, mbuzi aliyekomaa ni pungufu ya theluthi moja ya ng'ombe aliyekomaa.
Mbuzi-kaya, kama alivyo n'gombe, ni mnyama anayefugika. Hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa na ngozi yake. Kwani nyama na maziwa ni chakula, na ngozi kufanywa viatu, mishipi na mikoba pia.
Mbuzi-kaya hula majani, hucheua na kutafuna tafuna chakula chake mara kadhaa ilhali kikizunguka kati ya vyumba mbalimbali vya tumbo na mdomo wake kabla ya kukimeza kabisa, kama vile afanyavyo ng'ombe.
Mara nyingi mbuzi-kaya hubeba mimba na kuzaa mapacha kadhaa.
Mbuzi ni kati ya wanyama wa kwanza waliofugwa na binadamu. Kuna spishi za kufugwa na spishi za porini.
Faida za mbuzi
[hariri | hariri chanzo]Kuna faida nyingi za mbuzi aina hizo ni:
- (i) Hutupatia ngozi kwa ajili ya kutengenezea vitu kama viatu.
- (ii) Hutupatia nyama.
- (iii) Hutupatia kwato kwa ajili ya kutengenezea vitu kama vishikizo vya nguo.
- (iv) Hutupatia maziwa.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Goat breeds Archived 25 Septemba 2008 at the Wayback Machine.
- Goat resources
- Goat care and feeding guide Archived 11 Aprili 2016 at the Wayback Machine.
- Abraham Lincoln's sons kept pet goats inside the White House
- The American Dairy Goat Association Home Page
- Ruminations, The Nigerian Dwarf and Mini Dairy Goat Magazine
- American Goat Society
- Miniature Dairy Goat Association
- How to keep fires down in California scrub: Chew it.
- International Goat Association Archived 20 Mei 2007 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mbuzi-kaya kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.