Msitu wa mvua
Msitu wa mvua ni msitu unaopokea mvua nyingi yaani usimbishaji wa zaidi ya milimita 2,000 kwa mwaka. Kwa hiyo msitu unastawi vizuri kuna aina nyingi za mimea na wanyama kushinda misitu mingine.
Kuna namna mbili za misitu hii kutokana na halijoto:
- Misitu ya mvua ya kitropiki katika nchi za joto
- Msitu wa mvua penye tabianchi ya wastani.
Misitu ya mvua katika tropiki
[hariri | hariri chanzo]Misitu hii iko kwenye kanda ya ikweta duniani kati digrii za longitudo 10° kusini na kaskazini.
Maeneo makubwa yako hasa Brazil katika beseni ya Amazonas, Afrika katika beseni ya mto Kongo, Asia ya Kusini-Mashariki na kaskazini ya Australia.
Misitu hii imepungua sana kutokana na kukatwa kwa miti na upanuzi wa kilimo.
Misitu ya mvua penye tabianchi ya wastani
[hariri | hariri chanzo]Nje ya kanda ya tropiki kuna misitu ya mvua kwenye pwani la magharibi ya Amerika Kaskazini, Chile, Tasmania, New Zealand, Japani na kwenye magharibi ya Kaukazi.
Tabia za msitu wa mvua
[hariri | hariri chanzo]Ardhi na matatizo ya kilimo cha kisasa
[hariri | hariri chanzo]Misitu ya mvua huonyesha rutba kubwa lakini ardhi yenyewe mara nyingi inakosa rutba.
Hii ni sababu ya kwamba maeneo ya misitu ya mvua hayafai kwa kilimo. Kama miti inakatwa mvua nyingi huondoa minerali za ardhi na kuzipeleka mtoni. Ardhi yenyewe inachoka haraka na baada miaka michache mavuno hupungua kabisa. Hii imeonekana mahali pengi ambako maeneo ya misitu hii yaligeuzwa kuwa mashamba; baada ya miaka michache ya mavono mazuri wakulima waliopata shida ya kudumisha maisha yao. Kwa bahati mbaya mara nyingi wakulima wale wameendelea kukata miti zaidi wakiacha nyuma kanda la nusu-jangwa.
Wenyeji asilia waliolima katika misitu hii walitumia maeneo madogo madogo tu wakihamahama hivyo mashamba yao yalifunikwa kirahisi tena na miti ya karibu iliyozuia uharibifu wa ardhi.
Mzunguko wa minerali
[hariri | hariri chanzo]Miti na mimea inastawi vizuri kwa sababu majani pamoja na ubao wa miti inayoanguka chini na maiti za wanyama vinaoza katika unyevu haraka na kuwa chakula cha mimea tena. Harakati hii inasaidiwa na aina nyingi za uyoga zinazosaidia kuozesha haraka vitu vyote vyenya asili ya mimea au wanyama.
Uwingi wa spishi
[hariri | hariri chanzo]Imekadiriwa ya kwamba zaidi ya nusu, labda theluthi mbili za spishi zote za mimea na wanyama duniani hupatikana kwenye misiti ya mvua. Mamilioni ya spishi hazikutambuliwa bado.
Misitu ya mvua ya kitropiki imeitwa "duka la madawa ya dunia" kwa sababu kiasi kikubwa cha dawa asilia kutokana na mimea imepatikana hapo.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Msitu wa mvua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |